Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameanza mapema Kuliwania jimbo la Arusha Mjini kuwa Mali ya chama cha Mapinduzi na kuliondoa upinzani linakoshikiliwa na mbunge wa Sasa Godless Lema kupitia chama cha demokrasi na Maendeleo Chadema kwa kuwataka wanaccm waanze kujipanga vema kwenye Matawi yao
Gambo ambaye amekuwa akitajwa tajwa kutaka kuwania jimbo hilo bado hajatoa tamko rasmi kuwa anagombea ama la, ila amewataka wanachama wa ccm kuanza kupitapita kwenye matawi kwa lengo la kujiweka utayari.
"Kama kuna mwanachama yeyote wa ccm anaweza kufanya vurugu kwenye tawi lolote mwacheni afanye vurugu, lakini tukianza kuvutana ccm wenyewe kwa wenyewe hatufiki mbali "Amesema Gambo
Kauli hiyo ameitoa Mey 27 mwaka Huu katika shule ya msingi Nadosoito iliyopo jijini Arusha, wakati alipokuwa akiongea na wanachama wa ccm akiwa ameambatana na Mfanyabiashara Maarufu,Philemon Mollel ambaye aliwahi kuwa mgombea ubunge kupita ccm mwaka 2015
Aidha amesema kumekuwepo na Minong'ono kuwa jimbo la Arusha mjini huenda likagawanywa kwa maslahi ya wanasiasa, jambo ambalo amesema hakuna kitu kama hicho.
"Mlisema ukiweka jiwe na ccm watu wanachagua jiwe sasa mmechagua jiwe mmeona wenyewe " Amesema Gambo
Post a Comment