Serikali imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake wametakiwa kuomba upya wakizingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Mei 11, 2018
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini, Profesa Idris Kikula amesema
tangazo la Serikali namba moja la mwaka 2018 limesema maeneo yote
yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.
Amesema uamuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya
Madini ya mwaka 2010 ikisomwa na marekebisho yake ya mwaka 2017 na
kanuni ya 21 ya kanuni za Madini (Haki Madini za mwaka huu).
Amesema leseni zilizofutwa na wamiliki wake wanatakiwa
kuomba tena zinazihusu kampuni 11, kwamba leseni hizo zinajumuisha
migodi ya kati na mikubwa.
Migodi hiyo ni pamoja na Kabanga Nickel Company Limited,
National Mineral Development Corporation Limited, Bafex Tanzania Limited
ambayo inamiliki leseni za maeneo matatu.
Nyingine ni Mabangu Mining Limited, Resolute (Tanzania)
Limited, Wigu Hill Mining Company Limited, Nachingwea Nickel Limited na
Precious Metals Refinery Company Limited.
Post a Comment