Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa J’ amempongeza
mbunge mwenzake wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa kuhitimisha mafunzo
ya kisiasa na kusema sasa Sugu, anasubiri kuwa Rais wa Tanzania
Profesa J ametoa utabiri huo leo Mei 11, 2018 bungeni kabla
ya kuanza kuchangia kwa bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji ya
2018/19, ameanza kwa kusema
“Natoa pongezi kubwa sana kwa pacha wangu aka Sugu kwa
kuhitimu mafunzo huko ndani ambayo yameongeza ujasiri na CV yake ya kisiasa na
natumaini sasa hivi hatakuwa rais wa Mbeya bali anakwenda katika mchakato wa
kuwa Rais wa Tanzania huko mbeleni.”
Pongezi kama hizo, zimetolewa pia na mbunge wa viti maalum
(Chadema), Devotha Minja ambaye amesema kilichompata Sugu ni harakati za
ukombozi wa taifa hili.
Profesa J akichangia bajeti hiyo ya viwanda amesema mkoa wa
Morogoro ulikuwa na viwanda vingi lakini vingi vimeshindwa kujiendesha na
kushauri uchunguzi ufanyike, ili kuona wapi tumejikwaa.
Post a Comment