Waziri Mkuu, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
zote nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la usafi wa mazingira
katika maeneo yao la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael
Chegeni aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kutatua tatizo la usafi
wa mazingira pamoja na miundombinu hususani katika masoko hali ya kuwa
Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakusanya fedha nyingi bila kuboresha
maeneo na kukithiri kwa uchafu.
“Mheshimiwa
Spika Kupitia Bunge lako tukufu, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi
pamoja na Maafisa Afya wasimamie zoezi la usafi na kuboresha
miundombinu yote na utawapima kupitia zoezi hili,” amesema.
Waziri Mkuu amesema suala la usafi limekuwa likifanyika kila jumamosi ya
mwisho wa mwezi baada ya kuasisiwa na Rais Dkt. John Magufuli, hivyo
ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji hao wahakikishe maeneo yao
yanakuwa safi na miundombinu inayoweza kutumika wakati wote.
Post a Comment