Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua Warsha ya
Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018
Jijini Dodoma leo.
.............................. ..............
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla amesema Serikali
itaendelea kutekeleza sera ya Taifa ya Utalii kwa ushirikiano na wadau
katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za
maliasili na utalii nchini.
Dk.
Kigwangalla ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma leo wakati akifungua warsha
ya kitaifa ya mapitio ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka
2018.
Amesema
mafanikio ya sekta ya utalii yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa
Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 na juhudi za Serikali katika
kutekeleza sera hiyo.
“Sera
hiyo kwa ushirikiano na Wadau katika usimamizi, uhifadhi na matumizi
endelevu ya rasilimali za utalii, utangazaji katika masoko mbalimbali ya
utalii duniani na mazingira bora ya uwekezaji.
“Wote
tunaelewa ya kuwa Utalii ni moja wapo ya sekta zinazokua kwa kasi na
hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kupunguza
umasikini wa kipato”.
Amesema
ukuaji wa sekta hiyo, umedhihirika pale ambapo katika miaka ya hivi
karibuni mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka Dola za
Marekani bilioni 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni
2.2 mwaka 2017.
Amesema ongezeko
la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka
1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017.
Waziri
Kigwangalla amesema sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya
mapato yote ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings).
Akizungumzia
mambo yaliyowekewa mkazo katika rasimu hiyo amesema ni pamoja na
Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wote wa utalii katika kuhifadhi
rasilimali za utalii.
“Kuendeleza
rasilimali watu, kuimairisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa,
kuimarisha mnyororo wa thamani katika mazao ya utalii, kuongeza wigo wa
mzao ya utalii kama vile kuendeleza utalii wa fukwe na utalii wa
mikutano, kuweka mkazo katika kutangaza Tanzania kama kituo bora cha
utalii kimataifa.
“Napenda
kusisitiza kuwa, Sera hii itakuwa na nyenzo nyingine muhimu za
kuitekeleza ambazo ni Mkakati wa utekelezaji wa Sera na Progamu ya
Maendeleo ya Utalii nchini.
“Tayari
Wizara imeanza maandalizi ya awali ya kukamilisha nyenzo hizo na
mtashirikishwa kikamilifu katika kuziandaa na kuitekeleza wake,”alisema.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali
Gaudence Milanzi amesema sera ya Taifa ya Utalii iliyopo hivi sasa
ilifanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 1999 ambapo ni takribani
miaka 18 iliyopita.
Amesema
kwa kutambua hilo, Wizara iliona kuna umuhimu mkubwa kupitia upya Sera
hiyo ili kuhakikisha ukuaji wa Sekta ya Utalii nchini unaenda sambamba
na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani ikiwamo mabadiliko ya
teknolojia, kijamii, kiuchumi, kisiasa na kimazingira.
Aidha,alisema
kwa kuzingatia kuwa msingi mkuu wa kuandaa Sera yeyote ni
kuwashirikisha wadau ambao ndio watekelezaji wa Sera hiyo, mapitio ya
Sera hii, yameshirikisha wadau wote muhimu tangu hatua za awali.
“Kazi
hii ilipangwa kufanyika kwa awamu tano (5) ambazo ni kukusanya maoni ya
wadau katika kanda saba za Tanzania Bara na Zanzibar, uchambuzi wa
maoni na kuandaa rasimu ya Sera, kuwasilisha rasimu ya Sera kwenye
warsha ya kitaifa ambayo inafanyika leo na hatimaye kuandaa rasimu ya
mwisho ya Sera na Mkakati wa Utekelezaji,” alisema.
Warsha hiyo imejumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi wanaohusika maendeleo ya sekta ya utalii nchini.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua Warsha ya
Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018
Jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza katika warsha hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza katika warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii Deogracious Mdam akizungumza katika warsha hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa ESRF, Deodatus Sagamiko akizumza katika warsha hiyo.
ESRF ni moja ya wadau wakuu waliofadhili zoezi hilo la kuhuisha sera ya
taifa ya utalii.
Baadhi ya wadau katika wa warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
Meza kuu.
Wadau.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi
(katikati) akifurahia jambo na Naibu Katibu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce
Nzuki (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deogracious Mdam wakati Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 Jijini Dodoma leo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na mdau wa
utalii, Dk. Leaky Abdallah wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya
Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 Jijini Dodoma leo.
Baadhi ya wadau wa utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
(Picha zote na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)
Post a Comment