Mkurugenzi
Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akitoa
ufafanuzi mbele ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam
wakati akifungua mkutano wa kujadili nafasi ya Asasi za kiraia katika
chaguzi zijazo hapa nchini.
Asasi
za kiraia nchini zimetakiwa kujitoa katika kuhakikisha wananchi
wanashiriki kwa wingi katika chaguzi mbalimbali ikiwemo ya serikali za
mitaa na wa serikali kuu wa mwaka 2020.
Hayo
yamesemwa mapema leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa
Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga alipokuwa akifungua
mkutano wa wadau wa uchaguzi, wenye lengo la kujadili hali ilivyo kabla
ya kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo
mwakani.
Mzee
Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation akichangia mjadala
mapema leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Uchaguzi ulioandaliwa
na Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society.
Katika
Mkutano uliowakutanisha wadau kutoka Asasi mbalimbali za Kiraia,
Taasisi za elimu ya juu, vyama vya wafanyakazi, vyama vya dini mashirika
yanayoshughulikia amani nchini kujadili nafasi na wajibu wao kama azaki kuelekea chaguzi zijazo hapa nchini.
Bwana
Kiwanga amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika kupiga kura umekuwa ni
mdogo sana kwani 2010 wamepiga asilimia 43 peke yake na kwa mwaka 2015
ni asilimia 67 ya wananchi wote wenye sifa za kupiga kura.
Baadhi ya washiriki kutoka asasi mbalimbali za kiraia wakifuatilia kwa umakini mkutano.
Ameeleza kuwa hii inatokana na wananchi kutokuwa na imani na viongozi wanaochaguliwa kwani wanaamini hata usipopiga kura basi mgombea wa chama fulani atapita kwa njia yeyote ile, hivyo taasisi zinazohusika ikiwemo wizara ya tamisemi na NEC pamoja na ZEC kuboresha utendaji wao wa kazi ili kurejesha imani hiyo kwa wananchi.
Amesema kuwa
asasi za kiraia zina jukumu kubwa la kushirika katika mchakato kabla,
kipindi chenyewe cha uchaguzi na baada ya uchaguzi kwa kuwapa hamasa
wananchi lakini pia kuomba nafasi za uangalizi katika kipindi hicho.
Wageni waalikwa wakifuatilia mkutano kwa umakini.
Amesisitiza
uhalali wa kuwapata viongozi ambao ni matakwa ya wananchi kwani hii
inaweza kuleta kitu kizuri kwa kuwa atakuwa kapewa Baraka zote na
wananchi na pia watashirikiana nae kwa hali na mali kwa kuwa wanajua
ndio chaguo lao sahihi.
Kwa
upande wake Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation
amesisitiza uwepo wa amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya
uchaguzi kwani amani ndio msingi wa mambo yote.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa uchaguzi ulioandaliwa na shirika la
Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo
jijini Dar es salaam.
Amesema kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo inapotokea watu wanamchagua mgombea Fulani alafu matokeo yanabadilishwa na kupewa mtu mwingine hii sio sawa na inaweza kutowesha amani ya nchi
Lakini
pia hali ya mtu anatumia muda mwingi kwenye foleni ya kujiandikisha na
mwisho wa siku anaenda kupiga kura anaambiwa jina lako halipo kwenye
daftari hali hii inasababisha watu wengi kuacha kujiandikisha kupiga
kura na kupoteza haki yao ya msingi.
Post a Comment