PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DR. Mpango awajibu wabunge bajeti ya Ulinzi lazima iwe na ukomo
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema si rahisi bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ...

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema si rahisi bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kutowekewa ukomo

Akijibu hoja za wabunge Mei 14, 2018 waliochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2018/19, Dk Mpango amesema

“Kuna ushauri ulitolewa wizara isiwekewe ukomo hili si rahisi, fedha hazitoshelezi yako mahitaji mengi ambayo ni muhimu ambayo ninyi  wabunge mliyasemea kwa nguvu.”

“Mlisema maji, vifaa tiba, kilimo kuwa kwenye mtungi mmoja lazima uchukue kidogo,” amesema

Dk Mpango amesema Serikali itaendelea kuliwezesha jeshi kwa kadri rasilimali zinavyoruhusu

Amesema hadi Aprili, 2018 Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilikuwa limepata fedha za matumizi ya kawaida Sh307.9 bilioni

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top