PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAONGOZA WATALII WATAKIWA KUISAIDIA SERIKALI KUKUSANYA MAPATO YA UTALII
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Viongozi wa chama cha waongoza watalii wakifuatilia mada na maswali toka kwa wajumbe wa mkutano wa waongoza watalii uliofanyika katika uku...
Viongozi wa chama cha waongoza watalii wakifuatilia mada na maswali toka kwa wajumbe wa mkutano wa waongoza watalii uliofanyika katika ukumbi wa Manor Hotel mwishoni mwa juma hili



Baadhi ya waongoza watalii wakisikiliza uwasilishwaji wa mada katika mkutano wao mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Manor Hotel mwishoni mwa wiki
 
 
 Chama cha waongoza watalii nchini(TTGA), kimeombwa  kuisaidia serikali kwa kutoa taarifa za baadhi ya kampuni za utalii ambazo zimekuwa zikikwepa kulipa kodi na ambazo hazilipi malipo stahiki kwa waongoza watalii.
Afisa Utalii ofisi za Mkuu wa mkoa wa Arusha.Flora Basir alitoa wito huo, wakati akifungua mkutano mkuu wa TTGA na kueleza Serikali inathamini kazi za waongoza watalii kwani ndio wamekuwa wakiwapokea na kukaa muda mrefu na watalii lakini wanaweza kusaidia kuzuia kukwepwa kodi.

"waongoza watalii ni mabalozi wetu wakubwa wautalii,  serikali inajua changamoto zenu na inazifanyia kazi, ikiwepo malipo duni mnayolipwa lakini tunawaomba msaidie kutoa taarifa kwa wanaokwepa kulipa kodi "alisema.
Awali Katibu Mkuu wa TTGA, Emmanuel Mollel alisema licha ya wao kufanyakazi nzuri ya kuwapokea watalii na kuwasafirisha katika hifadhi za taifa na maeneo mengine ya utalii,bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa.

Mollel alisema ,wanachangamoto ya kutokuwa na mikataba ya kazi,malipo duni, huduma duni kwenye hoteli za hifadhini,kero ya malango ya kuingia hifadhini, matatizo ya kukamatwa na askari wa usalama barabarani wakiwa na watalii na utata wa leseni za kazi yao.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa TTGA, Khalifa Msangi, alisema wanashukuru sana hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa na serikali kutatua baadhi ya kero lakini kasi ni ndogo sana.

"hivi sasa Serikali inatambua kazi wetu na tunaushirikiano lakini tungependa hizi kero zetu zipatiwe ufumbuzi ili serikali ifikie lengo la kupata watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2020 kwani sisi ndio mabalozi wakubwa wa utalii"alisema
Akizungumza katika mkutano huo, Mhifadhi Utalii wa Hifadhi za Taifa ya Serengeti, Susuma Kusekwa alisema, shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) wameanza kufanyia kazi kero za waongoza watalii.

"kuna kero za kukamatwa ndani ya hifadhi kutokana na kupita njia ambazo hazitakiwi hasa kuelekea eneo la Ndutu kwenye mazalia ya Nyumbu tunalifanyia kazi na Serengeti tutajenga barabara mpya katika eneo hilo"alisema
Hata hivyo, alitaka waongoza watalii hao, kufanyakazi kwa waledi na wakati wote wanapokabiliwa na changamoto wawasiliane na viongozi wa hifadhi ili kusaidiwa badala ya kulalamika tena wakiwa na watalii.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top