PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAKAZI WA MEATU WATAKIWA KUDUMISHA UHIFADHI ILI KUNUFAIKA NA WAWEKEZAJI WA UHIFADHI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
 Picha mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhianomiradi nayodhaminiwa na FCF katika wilaya ya Meatu ambapo hafla hii ...







 Picha mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhianomiradi nayodhaminiwa na FCF katika wilaya ya Meatu ambapo hafla hii ilifanyika katika kijiji cha sakasaka wilayani Meatu hivi karibuni


Mwandishi Wetu,Meatu.

Serikali imewataka wakazi wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,kuendeleza uhifadhi ili kunufaika ni miradi ya maendeleo inayotolewa na Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), inayofanya kazi kwa niaba ya kampuni za Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) na Mwiba Holdlings Limited zilizowekeza katika wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Meatu, Dk Joseph Chilongani,alitoa wito huo juzi, wakati wa makabidhiano ya miradi  yenye thamani ya zaidi ya sh 86 milioni iliyofadhiwa FCF kwa vikundi na taasisi za umma wilayani Meatu mwaka 2017/18 hafla iliyofanyika katika kijiji cha Sakasaka.

Dk Chilongani alisema, wilaya hiyo, imebahatika kuwa na rasilimali za wanyamapori hivyo ni wajibu wa wananchi kuendelea kutunza rasilimali hiyo kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

"tumeshuhudia hapa vikundi vya kuweka na kukopa(VICOBA), vikipokea miradi yao sasa huu ni mfano mzuri kwa wananchi kuona umuhimu wa kuhifadhi mazingira na wanyamapori" alisema.


Alisema misaada hiyo, isaidie  jamii kutambua umuhimu wa uhifadhi na hivyo,kuacha tabia ya kuingizwa mifugo maeneo ya hifadhi, kukata miti ama kuharibu mazingira.

Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii FCF,Alfred Mwakivike,alisema  vikundi tisa vya VICOBA katika wilaya hiyo, vimepewa fedha za mtaji kiasi cha sh 40.4 milioni ili kuwezesha vikundi hivyo na wanachama kufanya shughuli za maendeleo.

"tumetoa zaidi ya milioni 15 kusaidia mradi wa afya zahanati ya Mwajidalala, ujenzi kituo cha michezo cha watoto wadogo mji mdogo wa Mwanhuzi na kusaidia mradi wa maji shule ya sekondari Mwandoya" alisema.

Meneja maendeleo ya jamii FCF  Nana Grosse -Woodley  alisema, licha ya misaada hiyo kwa vikundi vya VICOBA na taasisi pia wana miradi ya kupambana na ujangili katika eneo hilo na miradi mingine ya uhifadhi, Maji,Elimu, Afya na ufugaji nyuki.

Alisema lengo ya FCF iliyoanzishwa mwaka 1994 ni kuisaidia Tanzania na watu wake katika jitihada zao za uhifadhi wa mali asili ya nchi hii, kuishirikisha jamii inayoishi karibu au kuzunguka maeneo mbalimbali ya hifadhi.

"FCF tumekuwa tukitoa  ufadhili na kuwawezesha  kuibua miradi mbalimbali ya kuwapunguzia wananchi umaskini na pia kuwaondoa katika utegemezi wa kutumia mapori hayo, kufanya ujangili wa kuua wanyama, kuharibu misitu na kulisha mifugo ambayo huleta uharibifu wa mazingira" alisema

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top