Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Akizungumz a wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ Jijini Dar es Saalam jana.
...........................
Tanzania
ni miongoni mwa nchi 54 za bara la Afrika zitakazoshiriki katika
tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ linalotarajiwa kufanyika
nchini Ufaransa katika mji wa ‘Cherbourg’ mwezi Julai mwaka huu.
Tanzania
inashiriki tamasha hilo la kihistoria kwa mara ya kwanza ambapo itapata
fursa ya kutangaza utamaduni wake na vivutio vya utalii vya mambo ya
kale hivyo kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi
mbalimbali zinazohusika na tamasha hilo Jijini Dar es Saalam jana,
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, alisema tamasha hilo litatoa fursa pana kwa nchi kutangaza vivutio vyake ikiwemo vile vya Zamadamu.
“Kimsingi
tamasha hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa Tanzania kutangaza vivutio
vyake na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini, kila nchi itapewa banda lake la kuonyesha vivutio vyake , Tanzania naamini inakuwa na vivutio vingi vyenye kupendeza watalii kama vile Zinjathropus, Ngoma za makabila mbalimbali pamoja na nyimbo.
“Baada
ya tamasha hilo, kutakuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini na
ninaamini hata zile nchi ambazo hazina rekodi nzuri ya kuja Tanzania kwa
wingi zilizopo Bara la Asia zitaanza kuja,’’. alisema Kigwangla.
Alisema
tamasha hilo linalotarajiwa kuhusisha takriban nchi zote za bara la
Afrika, zaidi limelenga kutangaza tamaduni na vivutio mbalimbali vya
utalii vilivyopo katika mataifa yote yatakayoshiriki huku likitajwa
kuwa tamasha bora na kubwa la utalii pengine kuliko matamasha mengine
yote kutokana na kila nchi kujitokeza kuonyesha vivutio vinavyopatikana
katika mataifa yao.
“Tanzania
tunavyo vivutio mbalimbali tunavyotarajia kwenda kuvionyesha katika
tamasha hilo, ukiacha vivutio vya mambo kale, tuna bonde la Olduvai
Gorge na mengineyo, tunayoamini kuwa kupitia tamasha hilo tutaweza
kuyatangaza na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini” alisema Dkt.
Kigwangalla.
Hata
hivyo alisema baada ya kukamilika kwa tamasha hilo, Septemba mwaka huu
hapa nchini kutakuwa na tamasha la ‘Urithi wa Mtanzania’ linalotarajiwa
kufanyika kwa mara ya kwanza na litakuwa likifanyika kila mwaka
kuadhimisha urithi wa Mtanzania.
Alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi
mzima,
pia litatoa fursa kwa kila wilaya kutangaza vivutio vyake, huku
akizitaka kila wilaya kujiandaa na tamasha hilo, litakalotoa fursa pia
kwa mikoa na wilaya hizo kukuza utalii wa maeneo yao.
Waziri Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asngya Bangu akiongoza zoezi la utambulisho.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Akizungumz a wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ Jijini Dar es Saalam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax mabula akizungumza katika mkutano huo.
Picha ya pamoja ya Waziri Kigwangalla na washiriki wa mkutano huo.
Waziri Kigwangalla akifurahia jambo na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Post a Comment