Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 7 kwa
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kwa kushirikiana na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe kufanya Operesheni ya
kuwaondoa wavamizi wa nchi jirani wanaodaiwa kulima na kufuga ndani
kisiwa cha Izinga kilichopo ndani ya Pori la Akiba la Kimisi mkoani
Kagera.
Ametoa
agizo hilo jana wakati wa ziara yake wilayani Karagwe mkoa wa Kagera
muda mfupi baada ya kupokea taarifa na malalamiko ya kukamatwa kwa
mifugo ya Watanzania ndani ya kisiwa cha Mubali huku kukiwepo mazao
yanayodaiwa kulimwa na wananchi wa Rwanda katika kisiwa kingine cha
Izinga.
“Ndani
ya siku saba hicho kisiwa cha Zinga msafishe kila kitu, Mkuu wa Wilaya
msaidie mtengeneze kikosi kiende kule kitoe takataka zote zilizoko kule,
inakua ngumu kuadministrate (kutawala) wengine wa kwetu tunawatoa alafu
wa nchi nyingine wamekaa, unatawalaje?”. Aliuliza kwa mshangao Dk.
Kigwangalla.
Alisema watanzania wakienda upande wa Rwanda kuvua samaki ziwa Ihema wanauawa mara moja bila mjadala, wakati kwa upande wa Tanzani raia wa nchi hiyo wapo wengi na wengine wamepewa Uraia wa Kuasili (Citizenship by Naturalisation, CN) na huwa hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji wala mauaji jambo ambalo alisema ipo haja kama nchi kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.
Alisema watanzania wakienda upande wa Rwanda kuvua samaki ziwa Ihema wanauawa mara moja bila mjadala, wakati kwa upande wa Tanzani raia wa nchi hiyo wapo wengi na wengine wamepewa Uraia wa Kuasili (Citizenship by Naturalisation, CN) na huwa hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji wala mauaji jambo ambalo alisema ipo haja kama nchi kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David
Kenyata alisema atatekeleza agizo hilo la Waziri Kigwangalla kwa haraka
ndani ya muda uliotolewa ili kumaliza mgogoro huo.
Katika
hatua nyingine Waziri Kigwangalla alikataa ombi la Mbunge wa Jimbo la
Karagwe, Innocent Bashugwa la kuiomba Serikali iwamegee wananchi wa
vijiji jirani sehemu ya eneo katika Pori la Akiba Kimisi kwa ajili ya
shughuli za kilimo na ufugaji.
“Ardhi
mimi sitatoa, sjui mlima sjui nini, siwezi kwenda kupeleka hilo ombi
kwa Mhe. Rais, kabisa, hicho ni kitu ambacho hatuwezi kufanya kwa
sasa’,” Alisisitiza Dk. Kigwangalla.
Mbunge
huyo pia aliiomba Serikali kuweka uzio wa waya kwa ajili ya
kutenganisha mpaka wa hifadhi hiyo na vijiji kwa madai ya kuepuka
ukamataji wa mifugo ya wananchi unaofanywa na askari wa wanyamapori
kwenye ardhi za vijiji na kuingizwa hifadhini na kutozwa faini, hoja
iliyopigwa vikali na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka.
Hata
hivyo, Dk. Kigwangalla alikataa ombi hilo na kusema kuwa mipaka ya
hifadhi hiyo ni mikubwa kuwezesha utekelezaji wa ombi hilo. Alisema
Serikali itatengeneza mtandao wa barabara zinazounganisha hifadhi hiyo
na vijiji kwa ajili ya kuimarisha doria na shughuli za utalii pamoja na
kujenga ofisi ndogo za pori hilo katika kila wilaya inayohusika na pori
hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka aliwataka wananchi wanaofanya
vitendo vya kuingiza mifugo kwenye pori hilo wakati wa usiku kuacha mara
moja kwa kuwa wakimatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema
malalamiko ya wananchi hao kuwa askari wa wanyamapori wanakamata mifugo
yao kwenye maeneo ya vijiji na kuiingiza hifadhini kwa lengo la
kuwatoza faini kuwa sio ya kweli na kwamba malalamiko yanakuja kwakuwa
hukamatwa asubuhi wakiwa wameshatoka kulisha mifugo hifadhini.
Kisiwa
hicho cha Izinga ambacho kipo katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera
kina ukubwa wa Kilomita za Mraba 12 na kinapakana na nchi Rwanda.
Pori
la Akiba Kimisi lilianzishwa mwaka 2003 kwa Tangazo la Serikali na 116
na lina ukubwa wa kilomita za mraba 1,030. Pori hilo lina wanyamapori
mbalimbali wakiwemo Tembo, Twiga, Simba na Chui.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa
Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati
wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi
katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya
viongozi wa kijiji cha Mwisheni alipofika kukagua Pori la Akiba Kimisi
wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya
hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa
Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati
wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi
katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa
Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka wakati akikagua Pori la Akiba Kimisi
akiwa kwenye ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya
hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha mpaka wa Pori
la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi
kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana. Kulia ni
Mkuu wa Karagwe, Godfrey Mheluka na Mbunge wa Karagwe, Innocent
Bashungwa (kulia kwake).
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa
Wilaya ya Ngara, Lut. Col. Michael Mutenjele (kushoto) wakati wakivuka
kivuko cha Ruvuvu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kutatua migogoro
ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera
jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia baadhi ya
mifugo iliyokamatwa ndani ya Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake
ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya
Ngara mkoani Kagera jana.
(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).
Post a Comment