PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MHADHIRI WA TUMAINI DAR AIPINGA KAMATI YA MAADILI TFF KUWA NA UWEZO WA KUTHIBITISHA NYARAKA KUGHUSHIWA ZILIZOMHUKUMU WAMBURA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mhadhiri wa sheria chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam Edwin Mgandila ametoa maoni yake juu ya utaratibu uliotumika kusikiliz...


Mhadhiri wa sheria chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam Edwin Mgandila ametoa maoni yake juu ya utaratibu uliotumika kusikiliza shitaka la wambura na utaratibu upi unaotakiwa utumike

“Ni wazi kwamba kamati ya maadili ya TFF ina mamlaka ya kisheria na kimahakama,  kukiwa na organ yenye mamlaka ya kimahakama wakati wa kutenda haki inaongozwa na misingi ya kisheria kwa mfano msingi mmoja wapo ni wa kikatiba kwamba mtu anavyohukumiwa kuna mchakato wa kisheria ambao haukwepeki. Kama hiyo mamlaka ya maamuzi imetoa maamuzi ni lazima impe sababu za maamuzi yale hiyo ndio misingi ya kisheria.

“Inapokuwa imetokea hivyo kama kuna hatua za kukata rufaa na kuna vyombo vya kusikiliza rufaa vinaweza vikasikiliza rufaa  kama hakuna mchakato huo wa rufaa, wanaweza kwenda mahakamani kwa sababu kitu nachoweza kuwashauri TFF ni kurudia upya mchakato wa haki ya bwana Wambura na kufuata utaratibu wa kisheria siku zote kwa sababu hiyo hukumu ilikuwa ‘tainted na irregularity’ na hukumu ikiwa hivyo (‘tainted na irregularity’) ina madhara yake inapokuja suala la rufaa, inaweza ikaamriwa kufanya maamuzi upya kwa kuzingatia taratibu za kisheria au mahakama ya juu inaweza ikatengua yale maamuzi ya awali na kumtangaza yule mtu hana hatia au ameonewa.

“Sheria inasema kwamba, sio haki itendeke tu bali ni lazima bali ni lazima haki ionekane ikitendeka. Nimeufuatilia vizuri mchakato wa bwana wambura na kitu kingine nilichokifahamu ni tuhuma za kufoji unapozungumzia kufoji nyaraka hiyo ni miaka saba hadi 14 jela maana yake ni kosa la jinai, inapokuwa kosa la jinai ukiangalia shria ya ushahidi ya Tanzania inakwambia kwamba, yule anayekutuhumu ni lazima athibitishe.

“Kiwango cha kuthibitisha ni pasipo na shaka yoyote kwa hiyo pale walitakiwa wathibitishe pasipo shaka yoyote na kuthibitisha pasipo shaka yoyote sio jambo rahisi na watafanya hivyo iwapo mchakato mzima wa kisheria ulifuatwa, hiyo ndio position ya kisheria.

Kumekuwa na mkanganyiko kidogo, kamati ya maadili inaweza kujiridhisha kwamba kuhusu nyaraka kughushiwa au ilitakiwa ipeleke kwenye mamlaka nyingine yenye uwezo wa kuthibitisha halafu irudishe majibu kwenye kamati ya maadili?

“Ile kamati haina uwezo wa kuthibitidha hilo, kuna vitengo maalum vya polisi na kuna watu tunawaita mashahidi wa kiutaalam, inatakiwa atafutwe mtaalam kwa sababu jambo la kughushi ni kosa la jinai na mamlaka yenye uwezo wa kufanya uchunguzi wa kosa lolote la jinai ni polisi kwa hiyo suala ambalo lilitakiwa kupelekwa kwenye mamlaka husika.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top