PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MFUKO WA FIDIA NI MKOMBOZI WA WAFANYAKAZI NCHINI - WAZIRI MHAGAMA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Uteke...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2018 Bungeni Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kujadili Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2018/2019 kilichofanyika Mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akifuatilia uwasilishwaji wa makadirio ya bajeti ya Ofisi yake wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango ofisi hiyo Bw.Packshard Mkongwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika Machi 27, 2018 Bungeni Dodoma.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Amina Mollel akiuliza swali wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea akiuliza swali wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF Bw.Anselim Peter akiwasilisha mada kuhusu Utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2018.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika mjini Dodoma.

Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri  Mkuu wakiteta jambo mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora, Katikati ni Bi.Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu) na wa kwanza kulia ni Bw. Erick Shitindi (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria kupitisha Makadiri ya bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2018/19 kwa Fungu 25 na 37 Dodoma.

                (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)
Na MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi,Vijana,  Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameeleza kuwa uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni suala muhimu kuzingatia faida nyingi zitokanazo na mfuko huo tofauti na ilipokuwa awali.
Ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019 kwa mafungu 25 na 37 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.
Waziri Mhagama alieleza kwamba, miongoni mwa faida za uwepo wa mfuko huo ni pamoja na wafanyakazi kuwa na maisha bora kutokana na muendelezo wa kipato baada ya kupata ajali au kupoteza uwezo wa kufanya kazi, mazingira bora na yenye uhakika kazini na waajiri kupata unafuu wa kulipa gharama mbalimbali endapo mfanyakazi atapata janga kazini kwa sasa mzigo huu unabebwa na mfuko na kuwa na ongezeko la tija kazini kutokana na wafanyakazi kufanya kazi kwa ari pamoja na kuwepo kwa wingi kazini.
“Hakika mfuko huu ni mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi na waajiri wote kwa kuzingatia umekuja wakati mwafaka na umeongeza tija kwa kuwa malengo ya mfuko yanapelekea maisha bora kwa wafanyakazi na kuleta tija kuzingatia umuhimu wake”.Alisema Mhagama
Pamoja na hayo Waziri Mhagama aliwapongeza WCF kwa hatua nzuri ya kuanzisha mfuko huo wenye malengo chanya yatayosaidia kuongeza na kuendeleza azma ya Serikali ya kuwa na Uchumi wa Viwanda kwa kuwa wafanyakazi watakuwa na mazingira mazuri ya uzalishaji na ukuzaji wa uchumi wa nchi.
“Kipekee niwapongeze WCF kwa kuwa na mfuko huu, tunapaswa kuhakikisha unakuwa  endelevu na wa mfano kwani unasaidia kuleta chachu katika ukuaji wa uchumi na kuisaidia Serikali kufikia azma yake ya kuwa na Uchumi wa Viwanda”.Alisisitiza Mhagama
Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF Bw.Anselim Peter alieleza kuwa, mfuko unamajukumu mengi yenye malengo chanya ikiwemo kusaidia kubuni, kukuza na kuendeleza mbinu za kupunguza ajali katika maeneo ya kazi.
“Miongoni mwa majukumu ya mfuko huu, haikuwa kulipa fidia pekee bali kuwa na mbinu mbalimbali za kibunifu za kupunguza au kumaliza kabisa ajali katika maeneo ya kazi”.Alisisitiza Anselim.
Aliongeza kuw, kufanikisha hayo yote,michango ya wabunge ni muhimu katika kutoa uelewa sahihi wa madhumuni na uendeshwaji wa mfuko huo.
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea (Mb) alipongeza kazi nzuri inayofanywa na mfuko na kuwaomba kuwa pamoja na mfuko kujali wafanyakazi wawapo kazini ni vyema pia kuendelea kuhamasisha zaidi kwa kutoa elimu juu ya mfuko ili umma wa Watanzania kuelewa faida za mfuko huo.
AWALI
Workers Compensation Fund (WCF) ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Umma na Binafsi uliochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top