PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BMT YAITAKA TFF KUMALIZANA NA WAMBURA KABLA YANKULETA KESI ZAO BMT
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na George Mganga Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limeitaka TFF kumalizana na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Ric...



Na George Mganga
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limeitaka TFF kumalizana na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Richard Wambura.
Akizungumza na Radio One jana, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Mohammed Kiganja, alisema TFF ina Kamati zake maalum za kutenda kazi na kufanya maamuzi juu ya kile kinachomsibu Wambura hivi sasa.
Aidha ameongeza kuwa kama Wambura alishakata rufaa basi inabidi wamalizane wao kwa wao kwa kipindi hiki, na endapo itatokea ngazi za huko hakuna maelewano, watawasili BMT.
Hata hivyo taarifa iliyotoka jana  kutoka TFF kupitia Kamati ya Utendaji, ilithibitisha kumuengua Wambura kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Rais, na Athumani Nyamlani kutangazwa kukaimu nafasi hiyo.
Wambura alifungiwa na Kamati ya Maadili ambayo imeeleza kumkuta na hatia na makosa kadhaa yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya malipo ambayo yameelezwa hayakuwa sahihi
 
CREDIT: SALEHJEMBE BLOG 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top