PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RAISI MAGUFULI AMTEUA DR. KILANGI WA SAUT KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (AG)
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (A...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Taarifa iliyotolewa jioni hii na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Adelardus Kilangi unaanza tarehe 01 Februari, 2018.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St. Augustine University) kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA).

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Paul Joel Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG) kuanzia leo tarehe 01 Februari, 2018.

Kabla ya Uteuzi huu Bw. Ngwembe alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority – TIRA).

Kufuatia uteuzi huu Mhe. Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu kuanzia leo tarehe 01 Februari, 2018.

Wateule wote wataapishwa Jumamosi tarehe 03 Februari, 2018 saa 9:00 Alasiri.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

01 Februari, 2018

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top