PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: POLISI DAR YAMKAMATA MTEKAJI WA WANAWAKE NA MPORAJI MALI ANAYEJIFANYA FREEMASON
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa wamefanikiwa kumkamata Rajabu Muham...
Polisi Yamkamata Mtekaji wa Watu na Mporaji Mali
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa wamefanikiwa kumkamata Rajabu Muhamed maarufu kwa jina la Rajeshi mwenye umri wa miaka 25  ambaye anatuhumiwa kwa kuteka wamama, kuwabaka na kuwapora mali.


Kamanda Mambosasa amesema kuwa mtu huyo hutumia gari aina ya Fun Cargo akikutana na wanawake huwalazimisha kuingia kwenye gari hiyo na kisha kuwatisha yeye ni Freemason hivyo watoe mali zao wasipofanya hivyo huwatishia kuwakata sehemu zao za siri.

"Hutumia gari namba T 172 BLH aina ya Fun Cargo rangi ya Silver huwakamata wanawake, huwanyang'anya wafanyabishara wanaoendelea kufanya shughuli zao na akishawakamata huwaingiza kwenye gari yake kwa nguvu kisha kudai vitu mbalimbali ikiwa pamoja na kuchukua mabegi na baadaye huzunguka nao mtaani huku akiwatisha kuwa yeye ni Freemason na kuwa atawauwa na kuwanyonya damu, kitendo hicho hupelekea wa kina mama hao kukabidhi kila walichokuwa nacho lakini pia huwatishia wakatoa password  za benki chini ya tishio kubwa la kuwatoa uhai na kuwakata sehemu za siri, huyu ni mnyama wa kutosha ana sura za binadamu lakini ni mnyama" alisema Mambosasa

Kamanda Mambosasa aliendelea kusema kuwa Rajabu Muhamed ameshawafanyia vitendo vya kinyama wanawake wengi sana hapa mjini ikiwa pamoja na kuwabaka na kuwadhalilisha

"Anafanya vitendo vya unyang'anyi kwa kutumia nguvu na hasa kwa wanawake, ubakaji na unyanyasaji wa kila aina, amefanya vitendo vingi sana mjini hapa vya unyanyasaji wa kina mama anawateka anajifanya ni Freemason anawapeleka mahali anapowapeleka na kuwafanyia vitendo vyote vya kinyama. Huyu muhumi huyu na anachoniambia mimi kwamba ameacha lakini amewadhuru wanawake wengi sana hapa mjini na wachache wenye ujasiri walifika kuripoti na ndiyo tukafuatilia na kufanikiwa kumtia mbaroni jana usiku maeneo ya Kinondoni".

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top