Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Bitekoakizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Naibu
Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisikiliza maelezo
mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ,mara baada ya kuwasili katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Baadhi
ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Iringa wakinasa
kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kuhabarisha wananchi juu ya ziara ya
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko mkoani humo, Leo 19 Februari 2018.
Umati mkubwa wa wachimbaji wadogo katika mgodi wa mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa wakisikiliza hatma ya mgodi huo kutoka kwa Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika , Leo 19 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko aakikagua mashimo mbalimbali kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Iringa
Naibu
Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameagiza kufunguliwa
ndani ya wiki mbili mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya
Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa ili kuwarahisishia huduma
wachimbaji wadogo za kujiingizia kipato chao.
Mhe
Biteko ameyasema hayo wakati akizungumza na
wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara Mara baada ya kuwasili
mgodini hapo kukagua hatua za kiusalama zilizofikiwa tangu kufungwa kwa
mgodi huo 12 Februari 2018 kufuatia matukio matatu ya ajali ambayo
yalipelekea vifo vya wachimbaji wanne.
Mhe
Biteko akiwa ameambatana na Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Mhe Amina Masenza,
Kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa wa Iringa, Mkuu Wa Wilaya ya
Iringa Mhe Richard Kasesela na wataalamu Wa Madini kutoka Wizara ya
Madini ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kujiridhisha uhakika Wa
usalama Wa wachimbaji kuanzia Leo 19 Februari 2018 hadi kufikia 5
Februari 2018 mgodi uwe umeanza uchimbaji.
Alisema
kuwa kufunguliwa kwa mgodi huo kutaongeza kipato cha wachimbaji hao
huku akisisitiza wachimbaji hao pindi mgodi utakapofunguliwa kuzingatia
taratibu za usalama mgodini na kulipa kodi stahiki za serikali.
Alisema
kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuwanufaisha
wananchi kupitia rasilimali zao ikiwemo Madini ambapo Tanzania ni nchi
yenye fursa nyingi kwa uchimbaji Madini ilihali wananchi hawanufaiki
ipasavyo na rasilimali hiyo.
Mhe
Rais Magufuli ametuagiza kuwalea na kuwasimamia wachimbaji wadogo
nchini ili kutoka kwenye uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na
hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa ili uchumi wa nchi ushikwe na
watanzania wenyewe.
Alisema
kuwa wachimbaji hao wanapaswa kushirikiana na serikali kuwafichua waovu
wanaoiibia serikali rasilimali Madini kwa kuyatorosha kwenda sehemu
mbalimbali nchini na nje ya nchi pasina kulipa kodi.
"Jichungeni
na kujilinda wenyewe ili kila kinachopatikana serikali ijue imepata
kiasi gani na wachimbaji wameingiza kiasi gani na kisemwe hadharani,
ndugu zangu Rais anahangaika kuona kila eneo ambalo lina wachimbaji
wadogo wana rasimishwa na hatimaye wananufaika na madini yao, lakini
bado kuna watu wanatorosha madini" Aliongea kwa msisitizo Mhe Biteko na
kuongeza kuwa
"Na
Mimi nataka niwaambieni wale wote wanaofikiri katika serikali hii
inayoongozwa na Rais Magufuli wanaweza kupenya na dhahabu watafute jambo
jingine la kufanya maana jambo hilo limepitwa na wakati"
Alisisitiza
kuwa wamiliki wa leseni kote nchini wanapaswa kutunza kumbukumbu za
biashara nzima ya madini ikiwemo mapato na matumizi kwa muda usiopungua
miaka mitano kinyume na hapo kwa mujibu wa sheria watatozwa faini ama
kifungo jela
Kwa
upande wake Mhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza alisema kuwa
wachimbaji hao wanapaswa kutofanya kazi kwa mazoea huku akisisitiza
wachimbaji hao kuwa na ushirikiano na kupendana.
Post a Comment