Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi wkipata chakula cha mchana kupititia mfuko wa uhifadhi wa taasisi ya Friedkin conservation Fund(FCF) unaolenga kuwanufaisha jamii inayozunguka mradi huo. |
Wanafunzi wakipakuliwa chakula cha mchana ambacho kinahisaniwa na taasisi ya Friedkin conservation Fund(FCF) |
Kichanja cha kukaushia samaki kwa ajili ya kitoweo cha chakula cha mchana kwa wanafunzi wa shule zinzosaidiwa na taasisi ya Friedkin conservation Fund(FCF) |
Kampuni ya Utalii ya Mwiba Holdings ltd, imetoa kiasi cha sh 541
milioni katika kuchangia miradi ya maendeleo ambayo inateketezwa na
Jumuiya ya Wanyamapori ya Makao na halmashauri ya Meatu mkoa wa Simiyu.
Kampuni
hii, imewekeza shughuli za utalii na uhifadhi katika hifadhi ya jamii
ya wanyamapori ya makao ambayo inapakana na Mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro.
Meneja
wa miradi wa taasisi ya Friedkin conservation Fund(FCF) ambayo
inasimamia miradi ya kampuni ya Mwiba, Nana Grosse-Woodley amesema fedha hizo zimetolewa katika miradi mwaka 2017
pekee.
Alisema
miongoni mwa miradi ambayo kampuni hiyo, imechangia mifuko 3000 ya
saruji yenye thamani ya sh 48 milioni kwa ajili ya ujenzi wa miradi
jamii,imetoa kiasi cha sh 32.5 milioni kuchangia miradi ya elimu.
"katika
kipindi cha mwaka mmoja,tumetoa kwa vijiji 9 mgao jumla ya sh 89.2
milioni,tumetoa fedha za pango la ranchi kwa kijiji cha makao sh 80
milioni lakini pia tumetoa kwa halmashauri kodi pango sh 40
milioni"alisema
Alisema
kupitia shughuli za utalii, katika wilaya hiyo, wametoa kiasi cha sh
28.8 milioni kwa kijiji cha Iramba ndogo,kiasi cha sh 28.8 pia kwa
kijiji cha Mbushi ambapo pia kiasi kama hicho, kimetolewa kwa kijiji cha
Makao.
"kwa
ujumla tumetoa kias chah 541,043,519 mwaka jana pekee kama michango ya
maendeleo kodi na makato mbali mbali kutokana na shughuli za utalii na
uhifadhi"alisema
mwenyekiti
wa kijiji cha makao,Anthony Philipo alisema tangu kampuni ya Mwiba ianze kuwekeza katika kijiji chao kuna manufaa makubwa ambayo wanapata.
"wamekuwa
wakichangia miradi ya maendeleo, pia wanatoka mgao wa shilingi 3milioni
kwa vijiji vilivyopo ndani ya WMA kwa mwaka lakini pia kijiji chetu
karibuni, tulipata mgao wa sh 10 milioni"alisema
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema uwepo wa wawekezaji katika
sekta ya utalii katika mkoa wake, imekuwa ni faraja kwani licha ya
kutoa fedha kwa vijiji pia halmashauri husika zimekuwa zikinufaika
sambamba na serikali kuu kupitia kodi mbali mbali.
"mkoa
wa Simiyu sekta ya utalii imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya
wananchi na wito wa serikali ni kuhimiza maeneo yaliyohifadhiwa
yaendele kutunzwa na pia kuacha kufanya uvamizi ukiwepo wa mifugo kutoka
nje ya mkoa"alisema.
Post a Comment