Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kutokana
na ukosefu wa damu katika benki ya damu salama, Prosper Magali ameamua
kuhamasisha watanzania kuchangia damu kwa ajili ya kufikia malengo ya
benki ya damu kwa mwaka.
Magali
amefikia hatua hiyo baada ya mwaka 2015 kutokea kwa ajali dada yake
ambaye alihitaji damu ya haraka zaidi na kupatiwa damu kutoka benki ya
damu ila hakuweza kukaa sana na kufatiki ndipo familia ilipoamua
kuhamasisha kuchangia damu kila mwaka na 2018 ikiwa ni mara ya pili.
Meneja
wa Damu salama kanda ya Mashariki Dkt Avelina Mgesa amesema kuwa kwa
mwaka damu lita 450,000 inahitaji ila mwaka 2016 iliweza kupatikana lita
takribani 160,000 ambapo hazitoshelezi kwa mahitaji ya kila siku.
Nesi
kutoka Mpango wa Taifa ya Benki wa damu salama Catherine Kiure
akimuhudia moja ya wahamasishaji wa uchangiaji damu Prosper Magali
wakati wa uchangiaji damu unaoendelea katika Enep la Ubungo Plaza Jijini
Dar es Salaam.
Wananchi
wakiwa wamejitokeza kuchangia damu salama uliohamashihswa na Prosper
Magali kwa ajili ya kuhakikisha bnki ya damu inakuwa na damu ya kutosha.
Mwandishi wa MMG/Kajunason Blog Cuthbert Kajuna akiwa anachangia damu leo Jijini Dar es salaam.
Mwandishi
na mshereheshaji maaruf nchini Taji Liundi 'Master T' akiwa
anachukuliwa vipimo kwa ajili ya kuchangia damu katika benki ya taifa
ya damu salama nchini uliohamishwa na Prosper Magali.
Muhamasishaji
Prosper Magali akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea
kilichompelekea kuamua kuhamasisha uchangiaji wa damu baada ya kutokea
kwa ajali ya dada yake na kupelekea kuhitajika kwa damu haraka sana na
kuoma kuna ulazima wa kuhamasisha wananchi waweze kuwa na utamaduni wa
kuchangia damu.
Dkt
Avelina Mgesa ambaye ji Meneja Damu salama kanda ya Mashariki
akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kufurahishwa na hatua
aliyoamua Prosper Magali ya kuamua kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa
ajili ya kuhakikisha matarajio ya kufikisha malengo ya lita 450,000 za
mahitaji ya damu kwa mwaka.
Post a Comment