Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mgodi wa kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya maeneo ya uzalishaji madini ya dhababu kwenye kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Lindi
Kamishna
msaidizi wa madini kanda ya kusini Ndg Mayigi Makorobela ameagizwa
kuanzisha haraka ofisi ya Madini Wilayani Ruangwa ikiwemo kupeleka
wataalamu ili kurahisisha huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo
ikiwemo elimu ya usalama kazini.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa agizo hilo
leo tarehe 18 Januari 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo
Kata ya Megembekenyela wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Alisema
kuwa Wizara ya Madini imeamua kuanzisha ofisi hiyo kutokana na maagizo
ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa
aliyoyatoa hivi karibuni wakati alipokuwa ziarani Mkoani humo ambapo
alibaini kuwa wachimbaji wadogo wanapata kadhia kubwa kutokana na umbali
wa ofisi kwani wanalazimika kutumia zaidi ya kilomita 45 kuzifikia
ofisi za madini zilizopo Wilayani Nachingwea.
Alisema
kuwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa anawapenda wachimbaji wadogo
nchini ambao hata hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt
John Pombe Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alibainisha
kukusudia kuwanufanisha watanzania kupitia rasilimali zao ikiwemo
madini.
"Mhe
Rais Magufuli anataka wananchi wote wanaoishi karibu na mgodi kunufaika
na rasilimali zao, nyote mtakuwa mashahidi, tangu nchi iliporuhusu
uchimbaji wa madini hakuna manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania
badala yake madini yamekuwa yakinufaisha mataifa mengine ambayo baadaye
tunayapigia magoti kuyaomba msaada" Alikaririwa Mhe Biteko huku
akipigiwa makofi na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo
Mhe
Biteko alisema kuwa lengo la kuanzisha ofisi ya madini katika Wilayani
hiyo ya Ruangwa ni kuwarahisishia wachimbaji kuwa na jukumu moja la
kuchimba na kuuza rasilimali wanazozipata kwani watakuwa sehemu ya
kuchagiza maendeleo sambamba na kuinufaisha serikali kutokana na ulipaji
kodi.
Aliwasihi
wachimbaji hao kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya
Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwani tangu ameingia
madarakani katika kipindi kifupi ameimarisha nidhamu mpya kwa kila
mtanzania na usimamizi madhubuti wa rasilimali za Taifa.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko
ameipongeza kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini
Exploration & Mining Services (GEMS) ambayo ni kampuni ya wazawa kwa
kufanya kazi kwa kufuata vyema sheria na taratibu za uchimbaji.
Post a Comment