PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: KONGAMANO LA WANAHABARI NA WADAU WA UTALII LILIVYOFANA JIJINI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Picha ya pamoja na mgeni rasmi katika kongamano la wanahabari juu ya uandishi wa habari bora za utalii Kundi la wanahabari na  wadau ...
Picha ya pamoja na mgeni rasmi katika kongamano la wanahabari juu ya uandishi wa habari bora za utalii

Kundi la wanahabari na  wadau wa utalii wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo

Mjumbe wa bodi ya TAHOA na mkurugenzi wa hotel ya marera safari lodges and hotel akitoa mada kwa wanahabari juu ya uwindaji wa kitalii na faida zake kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla

Chrispine Mayandika ni Katibu wa chama cha wawindaji  cha Simba professional hunters association akitoa mada katika kongamano la wanahabari na utalii juu ya umuhimu wa uwindaji wa kitalii katika kujenga uhifadhi endelevu nchini

Wanakongamano wakifuatilia kwa makini juu ya mada ya uandishi bora wa habari za utalii uliokuwa ukiwasilishwa na Neville Meena ambaye ni  katibu wa jukwaa la wahariri katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha

meneja wa chemchem  hotel bwana Charles Sylvester kushoto na Bwana Ramadhani Ismail mwenyekiti wa jumuiya ya uhifadhi wanyama pori Burunge wildlife management area wakifuatilia mada katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kwa makini kongamano hilo
 Serikali imewaonya  watu wanaojihusisha  na vitendo vya ujangili na kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria .

Afisa Utalii mkoa Arusha,Frola Assey alitoa onyo hilo, wakati akitoa mada juu ya mikakati ya mkoa Arusha kuboresha Utalii,katika kongamano la utalii la waandishi wa habari na wadau wa utalii na uhifadhi lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Alisema Vitendo vya ujangili na uvamizi maeneo yaliyohifadhiwa vina athari kubwa katika dhana ya kukuza utalii nchini
"Arusha ndio kitovu cha utalii nchini hivyo serikali haitakuwa tayari kuona wachache wanataka kuvuruga utalii" alisema
Alisema serikali mkoa Arusha imejipanga kuendelea kuondoa kero zilizopo katika sekta ya utalii na nyingi zimepatiwa ufumbuzi.
Alizitaja baadhi ya kero zilizotatuliwa ni kuondolewa mlolongo wa tozo kwa watalii barabarani,kuondolewa tatizo za leseni za kufanya biashara za utalii na kuimarishwa ulinzi kwa watalii.
Hata hivyo Assey alisema wanahabari kuendelea kuandike vyema habari za Utalii na uhifadhi ili kukuza sekta ya utalii nchini.
"Sekta ya Utalii inaongoza kwa kulipatia taifa mapato mengi ya kigeni hivyo katika kuongeza pato hilo tunapaswa kuwa na waandishi wenye weledi ambao wataendelea kutangaza vuvutio vya utalii" alisema

Akitoa mada katika kongamano hilo Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nelvin Meena alisema wanahabari ni watu muhimu katika utalii lakini wanapaswa kujiendeleza kielimu.
"Kuna mambo mengi ya kitalii hayaandikwi  kwa ufasaha hivyo makongamano kama haya yanasaidia kuwajengea uwezo wanahabari" alisema
Mjumbe wa bodi ya chama cha wawindaji wa kitalii nchini(TAHOA) Hillal Daffi alisema kumekuwepo na dhana potofu kuhusu uwindaji wa kitalii kuwa una hasara kwa uhifadhi jambo ambalo sio sahihi.
Daffi alisema uwindaji wa kitalii ni dhana ya uhifadhi na unachangia kiasi kikubwa katika pato la taifa na hauna athari yoyote katika uhifadhi.
Meneja wa taasisi ya Chemchem Foundation,Charles Sylivester alisema katika eneo la burunge WMA bado kuna matukio ya uvamizi wamaeneo yaliyohifadhiwa na hivyo kuchochea ujangili wa nyama.

Sylvester alisema katika eneo hilo ambalo kampuni yao ya Chem chem imewekeza ni muhimu sana wananchi kusaidia jitihada za serikali za uhifadhi.
Mwenyekiti wa Burunge WMA Ramadhani Ismail alisema eneo lao ambalo linaundwa na vijiji 10 litaendelewa kuhifadhiwa kwa manufaa ya Taifa zima.
Ismail alisema WMA imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii kwani wananchi hawachangii tena miradi ya maendeleo kutokana na WMA kutoa fedha  hizo.
Kongamano hilo linashirikisha wanahabari 100 kutoka Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top