Picha ya pamoja na mgeni rasmi katika kongamano la wanahabari juu ya uandishi wa habari bora za utalii |
Kundi la wanahabari na wadau wa utalii wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo |
Mjumbe wa bodi ya TAHOA na mkurugenzi wa hotel ya marera safari lodges and hotel akitoa mada kwa wanahabari juu ya uwindaji wa kitalii na faida zake kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla |
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kwa makini kongamano hilo |
Afisa Utalii mkoa Arusha,Frola Assey alitoa onyo hilo,
wakati akitoa mada juu ya mikakati ya mkoa Arusha kuboresha
Utalii,katika kongamano la utalii la waandishi wa habari na wadau wa
utalii na uhifadhi lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Alisema Vitendo vya ujangili na uvamizi maeneo yaliyohifadhiwa vina athari kubwa katika dhana ya kukuza utalii nchini
"Arusha ndio kitovu cha utalii nchini hivyo serikali haitakuwa tayari kuona wachache wanataka kuvuruga utalii" alisema
Alisema serikali mkoa Arusha imejipanga kuendelea kuondoa kero zilizopo katika sekta ya utalii na nyingi zimepatiwa ufumbuzi.
Alizitaja baadhi ya kero zilizotatuliwa ni kuondolewa
mlolongo wa tozo kwa watalii barabarani,kuondolewa tatizo za leseni za
kufanya biashara za utalii na kuimarishwa ulinzi kwa watalii.
Hata hivyo Assey alisema wanahabari kuendelea kuandike vyema habari za Utalii na uhifadhi ili kukuza sekta ya utalii nchini.
"Sekta ya Utalii inaongoza kwa kulipatia taifa mapato mengi
ya kigeni hivyo katika kuongeza pato hilo tunapaswa kuwa na waandishi
wenye weledi ambao wataendelea kutangaza vuvutio vya utalii" alisema
Akitoa mada katika kongamano hilo Katibu wa Jukwaa la
Wahariri Nelvin Meena alisema wanahabari ni watu muhimu katika utalii
lakini wanapaswa kujiendeleza kielimu.
"Kuna mambo mengi ya kitalii hayaandikwi kwa ufasaha hivyo
makongamano kama haya yanasaidia kuwajengea uwezo wanahabari" alisema
Mjumbe wa bodi ya chama cha wawindaji wa kitalii
nchini(TAHOA) Hillal Daffi alisema kumekuwepo na dhana potofu kuhusu
uwindaji wa kitalii kuwa una hasara kwa uhifadhi jambo ambalo sio
sahihi.
Daffi alisema uwindaji wa kitalii ni dhana ya uhifadhi na
unachangia kiasi kikubwa katika pato la taifa na hauna athari yoyote
katika uhifadhi.
Meneja wa taasisi ya Chemchem Foundation,Charles Sylivester
alisema katika eneo la burunge WMA bado kuna matukio ya uvamizi
wamaeneo yaliyohifadhiwa na hivyo kuchochea ujangili wa nyama.
Sylvester alisema katika eneo hilo ambalo kampuni yao ya Chem chem imewekeza ni muhimu sana wananchi kusaidia jitihada za serikali za uhifadhi.
Sylvester alisema katika eneo hilo ambalo kampuni yao ya Chem chem imewekeza ni muhimu sana wananchi kusaidia jitihada za serikali za uhifadhi.
Mwenyekiti wa Burunge WMA Ramadhani Ismail alisema eneo lao
ambalo linaundwa na vijiji 10 litaendelewa kuhifadhiwa kwa manufaa ya
Taifa zima.
Ismail alisema WMA imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii
kwani wananchi hawachangii tena miradi ya maendeleo kutokana na WMA
kutoa fedha hizo.
Kongamano hilo linashirikisha wanahabari 100 kutoka Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga.
Post a Comment