Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam
.............................. .............................. .........
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie
BOUCLY wamekubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja cha kuchunguza
tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON
kuhusu ujangili wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani
Iringa.
Dk.
Kigwangalla na Mkurugenzi huyo, wamefikia makubaliano hayo leo Januari
2, 2018 wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara
ya Maliasili na Utalii, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.
Aidha,
Waziri Kigwangalla amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake inaandaa
mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii nchini na mapato
ikiwemo kuwashirikisha wananchi kuandaa mwezi maalum wa Urithi wa
Tanzania pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia za
kielektroniki katika vituo mbalimbali ya Utalii.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi huyo amemuahidi Waziri Kigwangalla kuendelea
kumpa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kuendeleza Utalii nchini
na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza naMkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP),
Bi. Natalie BOUCLY katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House
Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikilizaMkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP),
Bi. Natalie BOUCLY wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika ofisi
ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana naMkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP),
Bi. Natalie BOUCLY baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo
ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam
Post a Comment