Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wajumbe
wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati
akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na wajumbe
wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya mara
baada ya kuwasili katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa salamu za wabunge
wa Mkoa wa Mbeya wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Leo Disemba 3, 2017
amewasihi Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mkoa wa Mbeya kuchagua viongozi makini, weledi, wenye nidhamu na kipawa
cha uongozi.
Mhe
Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akitoa salamu za wabunge Wa Mkoa Wa
Mbeya kwenye Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo
katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya.
Alisema
kuwa wajumbe hao hawapaswi kuchagua viongozi kwa sababu ya kufahamiana,
Urafiki, Ujamaa au Undugu badala yake wanapaswa kuchagua viongozi wenye
maono na mtazamo chanya ili wawe mfano bora katika kukiimarisha na
kukijenga Chama Cha Mapinduzi.
Mbele
ya wajumbe hao Mhe Mwanjelwa kwa ushirikiano na wabunge wote Wa Mkoa Wa
Mbeya wamempatia zawadi ya Pawatila Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kwa
ajili ya Kilimo cha kisasa ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na ufanisi
Wa uongozi wake kama Mwenyekiti katika kipindi cha miaka mitano kuanzia
2012-2017.
Alisema
kuwa Zawadi hiyo inayogharimu fedha za kitanzania takribani Shilingi
Milioni Tano ni michango ya wabunge hao kwa Mwenyekiti huyo kutokana na
uhodari wake katika kuimarisha Chama katika Mkoa Wa Mbeya sambamba na
kuyavunja makundi yote yaliyokuwepo wakati Wa uchaguzi Mkuu Wa mwaka
2015.
Akifungua
Mkutano huo Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu Wa Mkoa
Wa Lindi Mhe Godfrey Zambi alimpongeza Naibu Waziri Wa kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa kwa kusafiri usiku wa manane kwa ajili ya kushiriki katika
Mkutano huo pamoja na kuwa na majukumu mengi ya kiserikali Wilayani
Songea Mkoani Ruvuma.
Zambi
alisema Kuwa kitendo cha Mhe Mwanjelwa kushiriki katika Mkutano huo
kimeonyesha mfano bora na umakini katika kuheshimu Chama Cha Mapinduzi
kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Kwa
upande wake Msimamizi Mkuu katika Mkutano huo Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira
na Walemavu Mhe Antony Peter Mavunde aliwataka wajumbe hao kuchagua
viongozi wenye uwezo Wa kuwasaidia wanachama na wananchi katika
kuchagiza shughuli za maendeleo.
Aidha, alisema uchaguzi huo unapaswa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi.
Post a Comment