Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbi wa Arusha
School kupewa mafunzo kabla ya kupatiwa mikopo ya halmashauri. Picha na
Ferdinand Shayo
|
Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbi wa Arusha
School kupewa mafunzo kabla ya kupatiwa mikopo ya halmashauri. Picha na
Ferdinand Shayo
|
Mkuu wa Wilaya ya Arusha
Gabriel Daqqaro akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 ya mkopo wa
kinamama iliyotolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha .Picha na Ferdinand Shayo
|
Na
Ferdinand Shayo,Arusha.
Jumla ya
Shilingi milioni 605 zimetolewa kama mkopo wa kuwanufaisha wajasiriamali
walioko kwenye vikundi vya kinamama na vijana pamoja na walemavu waliopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akizungumzia
mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Arusha Hanifa
Ramadhani amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kuwawezesha kinamama na vijana
kuondokana na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili ili kuinua uchumi .
Mkuu wa
Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amewataka Vijana ambao ni wasomi kujiunga
katika vikundi hivyo na kupata mikopo ili kujiendeleza kiuchumi badala ya
kusubiri ajira serikalini ile hali nafasi ni chache na wahitimu wa vyuo ni
wengi.
Post a Comment