PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAZINGIRA YA ASILI YA MLIMA KILIMANJARO YANAPOHIFADHIWA HUISAIDIA JAMII KUBWA KUNUFAIKA NA MAJI SAFI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
UHIFADHI wa Mazingiara kama huu katika baadhi ya maeneo yanayotengeneza msitu wa Mlima Kilimanjaro husaidia kuwa na vijito vingi...


UHIFADHI wa Mazingiara kama huu katika baadhi ya maeneo yanayotengeneza msitu wa Mlima Kilimanjaro husaidia kuwa na vijito vingi vya maji vinavyotiririsha maji kuelekea kwenye mito mikubwa, ambayo husafirisha maji hayo hadi kwenye maeneo mengine kwa ajili ya matumizi ya kilimo, mifugo na majumbani.


Utunzaji wa mazingira kama huu unapaswa kuwa moja ya vipaumbele kwa jamii zetu nchini ili kuziwezesha kuwa na uhakika wa mvua, maji safi kutoka kwenye vyanzo vya asili vilivyomo msituni.. 


Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini walifanikiwa kuona mazingira haya safi ya mlima Kilimanjaro walipoungana na makundi mengine ya wanachuo wa chuo cha diplomasia, chama cha kudumisha urafiki wa china na Tanzania pamoja na maaskari kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania walopopanda mlima kilimanjaro kusherehekea maaadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania december 9, 2017 makundi haya yote yalikuwa yakiongozwa na mkuu wa majeshi mstaafu na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa TANAPA George Waitara.
 
Safari hiyo iliyoratibiwa na TANAPA pamoja na KINAPA ilikuwa ya siku sita kuanzia tarehe 5/12/2017 mpaka 10/12/2017 amabapo walitumia lango kuu la Marangu kisha kituo cha mandara, Horombo na kibo na kuelekea kilele cha UHURU.







maji haya safi na salama hutiririka katika ya misitu ya mlima kilimanjaro hapa ni kabla ya kufikia kituo cha manadara


Water falls kama inavyoonekana pichani hutirirsha maji yanayokuja kutumia na wakazi wengi wa mkoa wa Kilimanjaro


Water falls kama inavyoonekana pichani hutirirsha maji yanayokuja kutumia na wakazi wengi wa mkoa wa Kilimanjaro

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top