NA: MWANDISHI WETU ARUSHA
Kongamano la
pili la utalii na amani ambalo hushirikisha wanahabari, wanafunzi na wadau wa
utalii nchini, linatarajiwa kufanyika mkoani Arusha, Januari 19,2018.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mratibu wa kongamano hilo la pili
kufanyika mkoani hapa, Andrea Ngobole alisema, kongamano hilo,
limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Shahanga sports promotion.
Ngobole alisema, lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kupinga vita ujangili na kuhamasisha uhifadhi endelevu ambao utashirikisha jamii.
Alisema katika kongamano hilo,wanahabari watajadili mchango wa vyombo vya habari katika kukuza utalii na vita dhidi ya ujangili pia umuhimu wa jamii kushiriki katika uhifadhi endelevu kwa maslahi ya taifa.
“kama
ilivyokawaida mada mbali mbali zitatolewa na wahifadhi, watafiti katika
masuala ya uhifadhi na utalii na pia waandishi wa habari waliobobea
katika masuala ya uhifadhi ”alisema.
Alisema
kongamano hilo pia litaambatana na mashindano ya riadha ya Tourism
Marathon ambayo pia yatafanyika Arusha kuhamasha utalii.
Mkurugenzi wa taasisi ya Alfredo Shahanga promotion, Alfredo Shahanga alisema wanariadha zaidi ya 200 wanatarajiwa kushiriki.
"kwa
ujumla kongamano la mashindano hayo ni sehemu ya tamasha la Arusha
tourism Festival ambalo linatarajiwa kuwakutanisha wanahabari, wadau wa
utalii na wanariadha "alisema
Wanahabari
ambao watashiriki kongamano hilo ni kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini,
Dar es Salaam, Mara na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii.
Na haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea katika kongamano la mwaka jana hapa mkoani Arusha
Post a Comment