Ofisi ya Bunge imesema haijapokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa
Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai alipotafutwa na MCL Digital leo
Jumapili Desemba 3,2017 ili kujua iwapo ofisi yake imepokea barua ya
Mtulia amesema hawajapokea.
Kagaigai amesema hakuna ofisi inayokuwa wazi usiku hivyo hawajapokea
barua ya Mtulia ambaye taarifa ya kujiuzulu kwake aliitoa kwa vyombo vya
habari jana Jumamosi Desemba 2,2017 saa mbili usiku.
Katika taarifa yake, Mtulia alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu kwa utashi wake bila shinikizo la mtu yeyote.
Mtulia ameeleza sababu za kujiuzulu ubunge na kuhama chama kuwa imetokana na uzoefu alioupata kwa miaka miwili ya ubunge.
“Nimebaini kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama
tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani na imefanya vizuri katika
mambo mengi ambayo sisi wapinzani tuliahidi kuyatekeleza,” alisema
Mtulia.
BUNGE LAKANA KUPOKEA TAARIFA ZA KUJIUZULU MTULIA
Title: BUNGE LAKANA KUPOKEA TAARIFA ZA KUJIUZULU MTULIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Ofisi ya Bunge imesema haijapokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo...
Post a Comment