Waziri Kalemani ametoa taarifa hiyo alipotembelea kiwanda cha kutengeneza trasfoma tanalec kilichopo jijini Arusha na amesema kuwa serikali imepata hasara kubwa kwa uingizwaji wa transfoma kutoka nje ambapo hivi karibuni ziliingizwa zaidi ya trasfoma ishirini zilizogundulika kuwa chini ya kiwango.
Mkurugenzi wa ufundi na huduma wakala wa umeme vijijini REA Bengiel Msofe amesema wamepokea agizo la serikali na wataanza kununua vifaa vya ndani kama walivyo agizwa na waziri mwenye dhamana.
Mkurugenzi wa TANALEC Zahri Salehe anasema wamejipanga kuzalisha transfoma elfu kumi ili kumudu soko la ndani naye mkuu wa mkoa wa arusha Mrisho Gambo anasema kama serikali ya mkoa watahakikisha wanasimamia utekelezezaji wa agizo hilo.
Post a Comment