Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kulia)
akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa
Wanyamapori-Mweka, Brightone Mbilinyi kuhusu mafunzo ya silaha
yanavyotolewa chuoni hapo katika mahafali ya 53 ya chuo hicho
yaliyofanyika jana katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya
asilimia 60 ya mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo. Wengine Pichani
ni Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada (wa pili kushoto) na Mkuu
wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho (wa nne kulia).
Na Hamza Temba-WMU
.............................. ....................
Katika
kutimiza azma ya Serikali kuboresha huduma za ukarimu kwenye sekta ya
utalii nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imekichagua Chuo cha
Usimamizi wa Wanyamapori Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro kwa ajili
kutoa mafunzo maalum kwa waongoza watalii nchini.
Mafunzo
hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kesho (Jumatatu) chuoni hapo yatakuwa
kwenye mfumo wa kujiendeleza na yamelenga kuwawezesha watoa huduma
katika sekta hiyo kupata sifa za kusajiliwa na kupewa leseni ya
kuendelea kutoa huduma hiyo kwa mujibu ya sheria ya utalii Na. 11 ya
mwaka 2008 kifungu cha 48.
Hayo
yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga katika mahafali ya 53 ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa chuo
hicho katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada
kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii.
"Katika
kutambua utaalamu na uzoefu wa chuo chenu, Wizara yangu imeichagua
Mweka kutoa mafunzo yatakayowawezesha waongoza watalii nchini kupata
sifa ya kusajiliwa (cheti) na kupewa leseni," alisema Naibu Waziri
Hasunga.
"Nimefurahi
kusikia kuwa mmeshajipanga tayari kuanza kutoa mafunzo hayo baada ya
kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo na kuainisha mapungufu kwenye
taaluma, ujuzi na mitazamo pamoja na kuandaa mtaala wa mafunzo hayo.
"Nitoe
wito kwa waongoza watalii nchini wajisaji ili wapate mafunzo haya
muhimu kwakua katika miaka michache ijayo hawataruhusiwa kutoa huduma
hiyo bila kutimiza masharti haya ya kisheria,” alisema Hasunga.
Alisema
tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa watalii wengi wanaokuja nchini
hupata taarifa kutoka kwa wenzao waliotembelea Tanzania ambao muda wao
mwingi wanakuwa na waongoza watalii kwenye maeneo ya vivutio.
"Hivyo
ni muhimu wapewe mafunzo maalum waweze kutoa huduma bora zaidi
zitakazowafanya watalii wafurahie ukarimu wao waweze kuwa mabalozi
wazuri wa kuutangaza utalii wetu watakaporudi nchini kwao" alisema
Hasunga.
Alisema
licha ya Sekta ya utalii nchini kuchangia asilimia 17 ya pato la taifa
na asilimia 25 ya fedha za kigeni (watalii milioni 1.28 na bilioni 2
mwaka 2016), mchango wake unaweza kukua zaidi kupitia mikakati
mbalimbali inayowekwa na wizara yake ikiwemo hiyo ya mafunzo ambayo
imelenga kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni mbili mwaka 2020 na
watalii milioni 8 mwaka 2025 pamoja na mapato ya dola za kimarekani
bilioni 20 mwaka 2025.
Akizungumzia
kuhusu mafunzo ya jeshi usu chuoni hapo, Naibu Waziri Hasunga aliuagiza
uongozi wa chuo hicho kuendesha mafunzo hayo muda wote wa masomo
tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hutolewa kwa wiki mbili katika kila
'semister'.
"Mafunzo
haya yasiishie tu kwa muda wa wiki mbili, ni matarajio yangu kuona
yanaendeshwa katika kipindi chote cha mafunzo ikiwemo wanafunzi kuvaa
sare za heshima za jeshi usu, kuwa na nidhamu ya kijeshi na muhimu zaidi
kuonyesha utayari na uwezo wa kukabiliana na wahalifu ikiwemo
majangili," alisema Hasunga.
Aidha,
alizitaka taasisi zilizopo chini ya Wizara yake kuajiri wananfunzi
wanaomaliza chuoni hapo ikiwa ni pamoja na kutumia fursa ya chuo hicho
mahiri kuwaongezea ujuzi wafanyakazi waliopo makazini.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho alimueleza
Naibu Waziri Hasunga kuwa Chuo chake kimeshafanya maandalizi yote ya
kuanza kutoa mafunzo kwa waongoza watalii nchini kama ilivyoagizwa na
wizara yake ambapo tathmini ya mahitaji ya mafunzo hayo imeshafanywa kwa
kuainishwa mapungu katika taaluma, ujuzi na mitazamo.
"Tumeshaandaa
pia mitaala ya mafunzo ambayo imezingatia kuondoa mapungufu
tuliyoyabaini, na tunatarajia kuanza mafunzo yetu ya kwanza kwa wapagazi
100 kwa muda wiki tatu kuanzia jumatatu ijayo (leo)," alisema Prof.
Kideghesho.
Alisema
ili kufanikisha mafunzo hayo chuo chake kimepokea msaada wa Shilingi
milioni 110 kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa
ajili ya kutoa mafunzo kwa wapagazi wanaotoa huduma katika mlima
Kilimanjaro, fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya mafunzo na tafiti
mbalimbali.
Mahafali
hayo ya 53 yalihudhuriwa pia na Balozi wa Nigeria nchini, Balozi
Sahabi Dada, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo hicho, Prof.
Faustin Bee, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mkuu wa Wilaya ya
Same, Harun Mbogo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Nebo Mwina,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos
Silayo na baadhi ya wawakilishi wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda.
Chuo
cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilianzishwa mwaka 1963 baada ya
azimio la Arusha mwaka 1961 ambalo lilitaka uwepo wa watu waliopewa
mafunzo kwa ajili ya kulinda na kusimamia urithi wa rasilimali za
Afrika.
Chuo
hicho ambacho huendesha mafunzo yake kwa vitendo kwa zaidi ya asilimia
60 kimepata ongezeko la wanafunzi kutoka 25 mwaka 1963/1964 hadi zaidi
ya wanafunzi 550 mwaka 2016/2017 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Malawi na Cameroon.
Aidha,
katika kipindi cha miaka 54 iliyopita chuo hicho kimeweza kufundisha
zaidi ya mameneja wa wanyamapori 8,000 kutoka nchi zaidi ya 50 duniani.
Chuo
hicho pia kimepewa tuzo na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama Kituo
cha Ubora wa Taaluma ya Usimamizi wa Wanyamapori (Centre of Excellence).
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto)
akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa
Wanyamapori, Mweka, Leonard Mgamba kuhusu mafunzo ya taaluma ya
wanyamapori yanavyofanywa kwa vitendo chuoni hapo. Wengine pichani ni
Balozi wa Nigeria nchini, Sahabi Dada (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya
ya Same, Mhe. Harun Mbogo (kushoto) na Mtenaji Mkuu wa Wakala wa Huduma
za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiwa ndani
ya handaki linalotumika kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika Chuo cha
Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti
wahitimu 224 wa kozi mbalimbali chuoni hapo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akikagua
gwaride la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda
mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa kozi mbalimbali ikiwemo
Shahada, Astashahada na Stashada katika taaluma za usimamizi wa
wanyamapori na utalii katika mahafali ya 53 yaliyofanyika chuoni hapo
jana katika Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya asilimia 60 ya
mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo na wahitimu 224 wa kozi
mbalimbali walitunukiwa vyeti.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akisalimiana
na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda ambao
walishiriki kwenye mahafali ya 53 ya Chuo cha Usimamizi wa
Wanyamapori-Mweka jana.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Prof.
Faustin Bee (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba
(katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Harun Mbogo (kushoto)
wakiteta jambo wakati wa mahafali ya 53 ya chuo hichao ambayo
yalifanyika jana mkoani Kilimanjaro.
Mkuu
wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Jafari Kideghesho
(kulia) akiwasilisha taarifa fupi kuhusu chuo hicho kwa Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) wakati wa mahafali ya
53 ya chuo hicho ambayo yamefanyika jana mkoani Kiliamanjaro. Wengine
ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chuo hicho, Prof. Faustin Bee (wa
pili kushoto) na Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto)
akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo cha Usimamizi wa
Wanyamapori-Mweka, Prof. Faustin Bee (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi,
Mhe. Kippi Warioba (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Harun
Mgogo wakati wa mahafali ya 53 ya chuo hicho ambayo yamefanyika jana
mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada.
Mkuu
wa Chuo chaUsimamizi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Jafari Kideghesho
(kulia) akiteta jambo na Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akipata
maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori,
Mweka, Ebenezer Mollel kuhusu mafunzo ya taaluma ya wanyamapori
yanavyofanywa kwa vitendo chuoni hapo. Wengine pichani ni Mkuu wa Chuo
hicho, Prof. Jafari Kideghesho (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Moshi, Mhe. Kippi Warioba.
Sehemu ya taswira ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipanda mti wa kumbukumbu chuoni hao.
Baadhi
ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi ya Wanyamapori Mweka, pembeni yao ni
mifupa ya miguu ya tembo katika chumba maalum cha mafunzo ya
wanyamapori.
Sehemu
ya wananfunzi 224 waliopewa vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka wakiwasili katika viwanja
kwa ajili ya mahafali ya 53 yachuo hicho yaliyofanyika jana katika
viwanja vya chuo hicho wilayani Moshi Mkoa wa Kiliamanjaro. Vyeti hivyo
vilitpolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga.
Gwaride
la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka wakitoa heshma
mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga (hayuko pichani)
Naibu
Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia)
akimtunuku cheti Mhitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori, katika
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka, Valentina Fiasco ambaye ni raia
wa Italia katika mahafali ya 53 yaliyofanyika jana chuoni hapo katika
wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof.
Jafari Kideghesho. Jumla ya wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa
vyeti.
Naibu
Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia)
akimtunuku cheti mmoja ya wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa
Wanyamapori, katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka wakati wa
mahafali ya 53 yaliyofanyika jana chuoni hapo katika Wilaya ya Moshi
Mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari
Kideghesho. Jumla ya wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti.
Naibu
Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akitoa
tamko la kuwatunuku kozi mbalimbali wananfunzi 224 wa chuo cha
Usimamizi wa Wanyamapori Mweka katika mahafali ya 53 ya chuo hicho
ambacho yamefanyika jana mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa chuo
hicho, Prof. Jafari Kideghesho, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Prof.
Faustin Bee (wa tatu kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi
Warioba.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo
(mwenye tai) na washiriki wengine katika mahafali hayo.
Post a Comment