Baada ya Band ya Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na
kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya wimbo wake kwenye wimbo
wa “Zilipendwa” Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)
Godfrey Mngereza ameongea yafuatayo.
“Unaweza kuitazama katika mitizamo mbalimbali lakini unapoangalia kwamba
wanaanza kushtakiana kimsingi ni taratibu ambayo inagusa sana mambo ya
haki miliki, kabla ya kuitumia kazi ya mtu ni vizuri ukamuona mwenye
kazi mkubaliane”
“Ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja kwa moja ni kosa, cha
msingi hata kabla ya kumuweka Mwanasheria ili kudai haki yako ni vizuri
ukawafata au ukawasiliana na alietumia kazi yako bila ruhusa…. katika
hili linalojitokeza sasa hivi ni swala la kuamshana kwamba kazi ya sanaa
ya mtu flani haina tofauti na mali ya mtu ya aina nyingine, huwezi
kutumia gari la mtu bila ridhaa yake” – Mngereza
Home
»
BURUDANI
»
HABARI ZA AFYA
»
HABARI ZA BIASHARA
» BASATA yaongea kuhusu Msondo Ngoma kumdai Diamond Milioni 300
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment