Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amezindua kampeni za
chama hicho za uchaguzi mdogo wa udiwani akiahidi iwapo kitachaguliwa
kitaondoa hali ngumu ya uchumi na ukiukwaji wa haki.
Zitto akizungumza katika Kata ya Kijichi mkoani Dar es Salaam,
Jumapili Oktoba 29,2017 amesema wananchi watumie uchaguzi mdogo katika
kata 43 nchini utakaofanyika Novemba 26,2017 kutuma salamu kwa CCM
kwamba hawaridhishwi na jinsi nchi inavyoendeshwa.
Amesema mtu akitaka kujua uchumi unasinyaa, aangalie alikuwa akipata shilingi ngapi na sasa anapata ngapi.
Zitto amewaomba wananchi wa Kijichi kumchagua mgombea udiwani wa ACT
Wazalendo, Edgar Mkosamali ili kuwe na mabadiliko kwenye baraza la
madiwani la Halmashauri ya Temeke.
Kiongozi huyo amelalamikia kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara akidai ni
ukiukwaji wa Katiba na sheria za nchi na pia kuwanyima wananchi haki ya
kukusanyika kwenye vyama vyao.
"Leo hii tunasubiri uchaguzi mdogo ndiyo tufanye mikutano ya hadhara.
Kama hupendezwi na haya yote, onyesha chuki yako kwa kumchagua
Mkosamali," amesema.
Zitto amesema chama hicho kikipewa ridhaa ya kuongoza Kata ya Kijichi
kitaifanya kuwa ya mfano katika kutatua kero zinazowakabili wananchi.
"Kwa udogo na uchanga wetu tutawapa utumishi uliotukuka. Tunataka kuifanya Kata ya Kijichi kuwa ya mfano," amesema Zitto.
Akizungumzia uongozi, Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Yeremia Maganja
amewaeleza wananchi kwamba Jeshi la Polisi limekuwa likiwanyanyasa jambo
ambalo ni ukiukwaji wa Katiba na sheria za nchi.
Maganja amesema lazima nchi iongozwe kwa misingi ya Katiba na sheria ili kuleta haki kwa jamii.
Mgombea udiwani katika kata hiyo, Mkosamali amesema anatambua matatizo yaliyopo na amejipanga kuhakikisha anayatatua.
Amesema hatalala bali atazunguka kila mahali kutafuta wafadhili kwa ajili ya kuleta maendeleo kwenye kata hiyo.
Home
»
Matukio
»
Siasa
» ZITTO KABWE AWATAKA WANANCHI KUTOICHAGUA CCM KATIKA UCHAGUZI WA MADIWANI KATA 43
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment