Wema ameweka wazi maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni baada ya dakika chache tangu kuachiwa kwa picha za kwanza za Mbunge huyo akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Wema ameandika "Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvuz zaidi....Utarudi
tena ukiwa na nguvu kuliko ulivyokuwa awali...Shujaa wetu. ... Picha hii
imenifanya nipate hisia. Sasa naweza andaa safari ya Nairobi kuja
kukuona.. Awali nisingeweza kuvumilia kukuona ukiwa kwenye maumivu".
Wema Sepetu ametajwa na Chama cha Chadema kama mmoja wa wahamasishaji
aliyeweza kuhamasisha watu kutoa michango kwa ajili ya matibabu ya
Mbunge Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa
risasi na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye gari lake nje ya makazi
yuke huko mjini Dodoma.
Post a Comment