Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakazi wa Kijiji cha Itigi, Kata ya Itigi waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Itigi, Kata ya Itigi waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya serikali wakati wa Mkutano wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Damwelu Kata ya Ipande.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji na Kata ya Kitaraka
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya serikali wakati wa Mkutano wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji na Kata ya Kitaraka
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji na Kata ya Kitaraka
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwasili Kijiji cha Damwelu Kata ya Ipande kwa ajili ya mkutano wa hadhara na wakulima na wafugaji.
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya serikali wakati wa Mkutano wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Na
Mathias Canal, Singida
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu amekemea vikali viashiria vya mgogoro kati ya wakulima
na wafugaji katika maeneo ya malisho na mashamba vinavyoanza kuchipuka na
kuibua hisia za sintofahamu.
Migogoro
ya wakulima na wafugaji huanza kwa majibizano ya mara kwa mara kati ya wananchi
wenyewe kwa kuingiliana katika maeneo yao jambo ambalo likipuuzwa ingali dogo
hukomaa na kupelekea serikali kutumia nguvu nyingi katika kulimaliza.
Akizungumza
na wakulima na wafugaji kwenye ziara ya kikazi katika vijiji korofi
vinavyochagiza mgogoro huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka
wananchi kuacha haraka kuibua hasira baina yao jambo ambalo linawezekana
kutatulika.
Aliwataka
wakulima ambao wamevamia katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya mpango wa
matumizi bora ya ardhi kuondoka haraka katika maeneo hayo na kutafuta maeneo
mengine kwa ajili ya kilimo kwani endapo kama watakiuka maelekezo hayo serikali
itachukua hatua dhidi yao.
Aliwataka
wakulima hao waliovamia maeneo hayo kufika ofisi ya Afisa Mtendaji wa kijiji
ili kubaini kama wanastahili kupatiwa maeneo mengine kutokana na kukutwa katika
maeneo hayo mara baada ya kuanzishwa sheria ya matumizi bora ya ardhi ya mwaka
2007.
Mhe
Mtaturu alisema kuwa Mgogoro wa kimaeneo ya malisho na mashamba ambao umeanza
kumea katika kipindi cha hivi karibuni Wilayani Manyoni unahusisha Vijiji
jirani vya Itigi Mjini, Doroto na Damwelu vinavyochangia maeneo hayo.
Alisema
kuwa ni lazima kila mwananchi kuwa wakala wa kuhifadhi na kutunza mazingira
katika maneo yanayotuzunguka ikiwa ni pamoja na kutolima katika maeneo ambayo
yamehifadhiwa au kupangwa kwa ajili ya mambo mengine.
Hata
hivyo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi kufatilia ili kubaini
aliyetoa maeneo ya wafugaji kwa wakulima ili achukuliwe hatua za kisheria kwani
jambo hilo lina dalili zote za rushwa na uhujumu wa maeneo.
Sambamba
na hayo pia Kaimu Mkuu huyo wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka wananchi kuelekea msimu wa kulima
mazao ya kipaumbele ambayo ni Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.
Aidha,
alisema kuwa pamoja na mazao hayo ya kipaombele lakini wanapaswa kuongeza kasi
katika kilimo cha mazao ya chakula na Biashara hususani mahindi, mtama, Dengu
na zao la Alizeti.
Aidha,
Mhe Mtaturu aliwashauri wafugaji
kupunguza idadi ya mifugo waliyonayo kwa kuuza na kununua au kujenga nyumba za
kuishi ikiwa ni njia mojawapo ya kuweza kukidhi maeneo ya malisho yaliyopo.
Post a Comment