Timu ya soka ya Mdori Fc ya wilayani Babati mkoa wa Manyara juzi, imetwaa ubingwa wa michuano ya Chemchem Cup ya kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori na kupiga vita ujangili baada ya kuichapa timu Manyara Fc magori 2-1.
Kutokana
na ubingwa huo, timu hiyo ilipewa zawadi ya fedha taslim 1.4 milioni
na kikombe vilivyotolewa na wadhamini wa michuano hiyo Chemchem Lodge,
ambapo timu 23 zilikuwa zikishiriki.
Katika
mchezo huo wa fainali, ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa
Manyara, Joel Bendela, timu ya Manyara Fc ndio ilikuwa ya kwanza kupata
goli dakika ya 34 lililofungwa na Hamad Nassaro.
Mdori
wakicheza kwa kuelewana walisawazisha goli hilo dakika ya 37 goli
ambalo lilifungwa na Ally Mido kwa shuti kali baada ya kuitoka ngome
ya Manyara Fc.
Kipindi
cha pili, Mdori walikianza kwa kasi na katika nadakika ya 59, Ally Mido
tena alifunga gori la pili baada ya kuwahada kwa chenga walinzi wa
Manyara Fc.
Akizungumza
baada ya kukabidhi vikombe na zawadi, mkuu wa mkoa, Bendela ambaye
kitaaluma ni kocha, alisema ameshuhudia vipaji vikubwa kwa timu
zilizocheza fainali.
Alisema
ili kuyapa hadhi mashindano hayo, ambayo lengo lake la kuhifadhi
wanyamapori katika eneo la hifadhi ya jamii ya burunge, timu zote 23
zinazoshiriki zinapaswa kusajiliwa.
"nawaagiza
viongozi wa chama cha soka mkoa wa manyara mliopo hapa mzisajili timu
zote zilizoshiriki mashindano haya ili yawe rasmi baadaye tupate timu
moja ya mkoa"alisema
Bendela
pia alieleza kumshukuru mkurugenzi wa Chemchem foundation, Nicolaus
Negre na watendaji wengine kwa kuanzisha mashindano hayo.
Akizungumza
wakati wa kutoa zawadi kwa washindi, Negre alisema lengo la mashindano
hayo ni kuhamasisha uhifadhi nakupiga vita ujangili.
"kama
mkitaka tuendelee na mashindano haya, lazima tupambane na majangili ili
wageni waendelee kuja kwenye eneo letu la hifadhi ya jamii wanyamapori
burunge"alisema.
Washindi
wa pili wa michuano hiyo, walipewa kikombe na fedha raslim sh 1
milioni, mchezaji bora nakipa bora walipewa zawadi ya sh 25,000 kila
mmoja sawa na timu yenye nidhamu.
Kwa upande wa mpira pete,timu ya Sangawe Fc ilitwaa ubingwa na kuzawadiwa sh 500,000.
Post a Comment