Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia)
akiwa katika kikao na Maafisa Waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) alipofanya ziara ya kukagua utendaji ambapo aliwataka kuchukua
hatua dhidi ya watumishi wasiowaaminifu wanaolikosesha Taifa mapato
stahiki.
Meneja
wa Idara ya Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bandari ya dar es
Salaam, Bw. John Micah (kulia) na Meneja anaye husika na suala la
Mafuta Bw. Stephen Malekano (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) alipofanya ziara
Idara ya Forodha, Bandarini, Jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Forodha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), bandaro ya dar es Salaam,
Bw. John Micah, akifafanua jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), alipofanya ziara ya
kushitukiza bandarini, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili
kushoto) akitoa maelekezo kwa Maafisa waandamizi wa Mamlaka ya mapato
Tanzania-TRA, alipofanya ziara ya kushitukiza bandari ya Dar es Salaam
na kuagiza kitengo cha ukaguzi na upimaji wa mizigo bandarini kifumuliwe
baada ya watumishi wake kutofanyakazi ya kukusanya mapato ya Serikali
ipasavyo
Afisa
Kitengo cha Bandari Majahazi, Bw. Mahmood Makame, akifafanua jambo
mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)
(kushoto) kuhusu changamoto ya elimu kuhusu masuala ya kodi kwa wateja
wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kushitukiza
katika ofisi hiyo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya
Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza
katika Kituo cha Forodha Bandarini, kilichoko katika Bandari ya Dar es
Salaam na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kufanya mabadiliko
makubwa ya watumishi walioko katika idara ya upimaji na ukaguzi wa
mizigo baada ya kubainika kuwa baadhi yao wanajihusisha kwa namna moja
au nyingine na upotevu wa mapato ya Serikali.
Dokta
Mpango ametoa muda wa siku saba kwa TRA kumpa taarifa kamili ya
utekelezaji wa maagizo hayo, ikiwemo kuwahamisha watumishi wote waliokaa
muda mrefu kwenye eneo hilo la upimaji na ukaguzi wa mizigo ili
kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali katika Bandari hiyo.
Ameshangazwa
na kitendo cha Mapato katika Bandari ya Dar es Salaam kutoongezeka
licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano,
kuboresha Bandari hiyo kutokana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu
kushirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi ya
serikali.
“Pamoja
na kuwepo kwa mitambo ya kukagua mizigo (Scanners), baadhi ya bidhaa
zinakadiriwa kodi ndogo ikilinganishwa na thamani ya mizigo huku mizigo
mingine ikiwa si ile iliyotajwa kuwemo kwenye makontena na hupitishwa na
watumishi wasio waaminifu” alisisitiza Dokta Mpango.
Aidha,
Waziri huyo wa Fedha na Mipango ameuagiza ungozi wa TRA kuhakikisha
kuwa wanaongeza mapato katika bandari ya majahazi kutoka wastani wa
mapato ya shilingi bilioni 3.5 kwa mwezi hadi shilingi bilioni 5,
kulingana na malengo yaliyowekwa baada ya kubainika kuwa kuna ukwepaji
mkubwa wa mapato ya Serikali katika eneo hilo.
Dokta
Mpango ameuambia uongozi huo wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kuhakikisha
kuwa Bandari ya Majahazi ianze mara moja kutumia mfumo wa kukusanya
mapato ujulikanao kama TANSIS ili kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi.
Aidha,
ameviagiza vyombo vya dola kuwachunguza watumishi wote wakiwemo wa
ngazi za juu katika idara ya forodha bandarini na kuwachukulia hatua
kali wale wote watakao bainika kujihusisha na vitendo vyovyote
vinavyoikosesha Serikali mapato yake.
Post a Comment