Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Alhaj
Abdallah Bulembo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea
nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo.
Bulembo aliwahi kusema kuwa hatogombea tena lakini baadaye aliamua
kuchukua fomu. Hata hivyo Bulembo amesema aliamua kuchukua fomu ya
kugombea baada ya kupata shinikizo kutoka kwa makatibu wakuu na wazee wa
jumuiya hiyo.
"Sasa leo(Jumanne) nimewaita kuwaeleza sitagombea tena licha ya kuchukua
fomu, naamini wagombea 48 waliopatikana, kuna mmoja atatufaa kuongoza
jumuiya hii, leo ninapeleka barua kwa katibu mkuu wa chama (Abdulrahiman
Kinana) ya kumweleza dhamira yangu hii,” amesema Bulembo leo Jumanne
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Bulembo amesema uchaguzi katika ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia
Novemba 20 hadi 23, wagombea wote wapo lakini yeyote aliyeanza kampeni
mapema huyo ameshajikata," amesema.
Kuhusu hoja ya kuchukua fomu amesema haikuwa dhambi kwa kuwa kanuni za
chama zinaruhusu na upo uwezekano wa kuwa na nafasi mbili za uongozi.
"Kumekuwa na upotoshaji kwamba, ukiwa mbunge au waziri hauwezi kugombea
nafasi nyingine, sasa hapa nina kitabu cha kanuni za mwaka 2005, 2010,
2012 na 2017 zinasema kiongozi au mbunge, waziri anaweza kugombea ila
kamati kuu ya chama itaamua inavyofaa, kama bado anahitajika atapitishwa
lakini mie sitagombea tena,” amesema.
Home
»
Matukio
»
Siasa
» Bulembo Awasilisha Barua ya Kutogombea Nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment