PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Watu Wawili Wafariki Dunia Katika Maandamano ya Uchaguzi Kenya...Picha za Vurugu Hizi Hapa
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Watu wawili wameuawa wakati wa vurugu akikabiliana na maofisa wa polisi katika ngome ya upinzani ya Mathare, Mji Mkuu w...


Watu wawili wameuawa wakati wa vurugu akikabiliana na maofisa wa polisi katika ngome ya upinzani ya Mathare, Mji Mkuu wa Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa walisikia milindimo ya risasi zikifyatuliwa wakati wa makabiliano hayo ambayo yalisababisha vifo hivyo.


Afisa Habari wa Shirika la Habari la Uransa, Agence France-Presse (AFP), limeeleza kuwa, waliouawa walikuwa miongoni mwa kundi la waandamanaji katika eneo hilo ambao walikuwa wakipambana na kikosi maalum cha kuzuia ghasia hizo.

”Tumeambiwa kwamba wengi wao walikuwa wezi ambao walitumia fursa hiyo na hawakuweza hata kuwaheshimu polisi”, alisema ofisa huyo.


Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu ili kumpokonya ushindi.

Mataili yakichomwa barabarani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top