Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wanne kushoto) akishukuru
kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka
kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (watano kushoto)
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wapili kushoto) akishukuru
kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka
kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng Deusdedit Kakoko (watatu kushoto).
Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashuka 900
yenye thamani ya Sh. Milioni Kumi kwa Hospitali za Temeke, Mbagala
Zakheim na Round zilizopo katika Wilaya ya Temeke.
Msaada
huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit
Kakoko kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva ikiwa ni sehemu
kutambua na kuthamini dhamira na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli, ya kufikisha huduma
mbalimbali za kijamii kwa wananchi wote na hasa wa hali ya chini.
“Menejimenti
ya TPA, chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Bodi ya
Wakurugenzi ya TPA, inaunga mkono kwa dhati kabisa juhudi za Serikali ya
Awamu ya Tano za kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu, TPA inayo
Sera ya Misaada kwa Jamii ambayo imejikita katika kusaidia jamii kwenye
nyanja za Afya, Elimu na Maendeleo ya Kijamii,” amesema Mhandisi Kakoko.
Mhandisi
Kakoko ameongeza kuwa pamoja na kwamba TPA kazi yake kubwa ni kuhudumia
shehena mbalimbali zinazopita kwenye bandari zote nchini, lakini pia
ina wajibu wa kurudisha kile inachokipata kutokana na huduma zake kwa
kuisaidia jamii inayoizunguka na ndio maana imeamua kutoa msaada huo kwa
Wilaya hii ya Temeke ilipo Bandari ya Dar es Salaam ambayo kiutendaji
ndiyo bandari kubwa kuliko bandari zote hapa nchini.
Hivi
karibuni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli alizindua rasmi kuanza kwa kazi ya maboresho ya
Bandari ya Dar es Salaam na mara itakapokamilika mwaka 2022 itaiwezesha
bandari hiyo kuhudumia meli zenye uwezo wa kubeba kontena 8,000 kutoka
kontena 2,500 za sasa na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya
ushindani na kuliongezea Taifa mapato.
Post a Comment