PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TLS Imewataka Mawakili Nchi Nzima Kutoenda Mahakamani Jumanne na Jumatano
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limewataka mawakili nchi nzima kutokwenda mahakamani Jumanne na Jumat...


TLS Imewataka Mawakili Nchi Nzima Kutoenda Mahakamani Jumanne na Jumatano
Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limewataka mawakili nchi nzima kutokwenda mahakamani Jumanne na Jumatano kama njia ya kupinga Kampuni ya Immma Advocate kuvamiwa.

Akizungumza leo Jumapili, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema uamuzi huo umefikiwa jana na kikao cha baraza la uongozi la chama hicho.

Amesema mawakili wote wanaotetea wananchi kwenye mahakama na kwenye mabaraza wasifanye kazi siku hiyo.

Amesema baraza hilo linafahamu kwamba wateja wao wataathirika siku hizo lakini usalama wa mawakili ni muhimu zaidi.

Lissu amesema baraza la uongozi linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwahakikishia ulinzi mawakili wa Immma Advocate dhidi ya vitisho vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.

Amesema baraza hilo linafanya jitihada za haraka za kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Idara la usalama ili kujadiliana kuhusu shambulio hilo.

Lissu amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama,uhuru na heshima ya wanasheria na mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuwatetea wananchi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top