Akizungumza leo Jumapili, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema uamuzi huo umefikiwa jana na kikao cha baraza la uongozi la chama hicho.
Amesema mawakili wote wanaotetea wananchi kwenye mahakama na kwenye mabaraza wasifanye kazi siku hiyo.
Amesema baraza hilo linafahamu kwamba wateja wao wataathirika siku hizo lakini usalama wa mawakili ni muhimu zaidi.
Lissu amesema baraza la uongozi linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwahakikishia ulinzi mawakili wa Immma Advocate dhidi ya vitisho vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.
Amesema baraza hilo linafanya jitihada za haraka za kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Idara la usalama ili kujadiliana kuhusu shambulio hilo.
Lissu amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama,uhuru na heshima ya wanasheria na mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuwatetea wananchi.
Post a Comment