JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21
Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Japan (JICA),Bwana Shinichi Kitaoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika
Mazungumzo hayo Bw. Kitaoka amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi mzuri na
wa mfano hususani katika kupambana na rushwa na msukumo mkubwa anaoutoa katika
maendeleo hususani katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Jitihada zinazosaidia kuimarisha uchumi na kuboresha
huduma za kijamii na kuahidi kuwa JICA itaendelea kuwa mshirika mkubwa wa
maendeleo kwa Tanzania.
Bw.
Kitaoka ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea Tanzania kama Rais wa JICA
amemuahidi Rais Dkt Magufuli kuwa miradi yote ya maendeleo ya nyuma na ya sasa
inayotekelezwa kwa pamoja kati ya
Tanzania na JICA itamalizika kwa wakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa
barabara za juu (Flyover) wa TAZARA
unaoendelea kujengwa hivi sasa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwenge - Moroco
yenye urefu wa kilomita 4 nukta 3 pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja la
Gerezani.
“Tumefikia makubaliano mazuri kuhusiana na
miradi tunayoendelea kuitekeleza hapa nchini na wananchi watarajie kuona kazi
zikifanyika kuanzia mwezi june,mwakani hususani katika ujenzi wa daraja la
gerezani na mingineyo”
Kwa
upande wake Mhe. Dkt Rais Magufuli amemshukuru Rais huyo wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japan Bw. Shinichi Kitaoka kwa uamuzi wake wa kuja
Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania inatambua mchango mkubwa ambao Japan
inautoa katika maendeleo ya Tanzania kupitia JICA, na kwamba itaendeleza na
kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Japan katika masuala mbalimbali.
Mhe.
Rais Magufuli ameishukuru JICA kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi
mikubwa ya ujenzi jijini Dar es Salaam ikiwemo upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco,
utakaoiwezesha barabara hiyo kuwa na zaidi ya njia nane, ujenzi wa barabara ya
TAZARA, ujenzi wa Daraja la Gerezani njia nne, na barabara ya Bendera tatu hadi
Kamata.
“Tunathamini sana mchango unaotolewa na walipa
kodi wa Japan kupitia JICA katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini na
ninakuomba kuangalia uwezekano wa kufadhili na kujenga miundo mbinu na miradi
mbalimbali ya maendeleo katika Makao Makuu ya nchi Dodoma ambako serikali
imedhamiria kuhamia huko ili kuweka alama ya urafiki na mahusiano mema yaliyopo
kati ya Tanzania na Japan”
Mazungumzo
hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida,Katibu
Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Doto James, Katibu Mkuu Ujenzi Mhandisi Joseph
Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Mhandisi Patrick
Mfugale.
Emmanuel
Buhohela,
Mwandishi
wa Habari,Msaidizi wa Rais,
Dar
es Salaam.
21
Agosti, 2017
Post a Comment