PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MKURUGENZI APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJIPATIA MILIONI 336 KWA UDANGANYIFU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
      Mkurugenzi  wa Kampuni ya Candy& Candy, Josiah Kiman Kairuki(38), Mkazi wa Mikwecheni Jijini Dar es Salaam juzi alipan...
 

 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy& Candy, Josiah Kiman Kairuki(38), Mkazi wa Mikwecheni Jijini Dar es Salaam juzi alipandishwa tena Kizimbani, katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Longido, mkoa wa Arusha, kujibu tuhuma za kujipatia kiasi cha sh 336 milioni   kwa njia ya udanganyifu, baada ya kudai  kuwa ana kontena  la simu za I Phone 7 limezuiwa katika bandari ya Dar es Salaam.

Kairuki ambaye ni Raia wa Kenya , Julai 26 mwaka huu,   mahakama ya hakimu mfawidhi wa wilaya ya Longido, ilimwachia huru katika shitaka  hilo la kujipatia fedha hizo kwa njia ya  udanganyifu, kutoka kwa  Yusuph Mohamed  kutokana na maombi ya Jamuhuri yaliyowasilishwa mahakamani na Mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa polisi Anastazia  Mutatina.

Hata hivyo Kairuki, baada ya kuachiwa huru na Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Aziza Temu, alikamatwa na polisi akiwa nje ya mlango wa mahakamani na kurejeshwa kituo cha polisi cha wilaya ya Longido kwa mahojiano zaidi.

                           Kufikishwa tena mahakamani.

Mkurugenzi huyo juzi, aliunganishwa  na  Abdinasiri Adamnuru  na mbele wa hakimu mfawidhi wa wilaya ya Longido, Aziza Temu, walisomewa   mashitaka mawili kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu na kosa la pili lilimuhusu Adamnuru kujifanya afisa forodha Tanzania.

Mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa polisi Anastazia Mutatina alisema, watuhumiwa hao, walifanya makosa hayo,  kati ya Januari 23 na june 10, 2017 na upelelezi wa shitaka hilo bado haujakamilika.

Hata hivyo, aliomba watuhumiwa hao, wasipewe dhamana kutokana na kiasi kikubwa cha fedha wanachotuhumiwa  na pia wote kutokuwa na  makazi wa kudumu.

Hakimu Temu alikubali maombi ya upande wa mashitaka na watuhumiwa hao, walirejeshwa katika mahabusu ya Kisongo Arusha hadi August 23 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.        
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top