PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: KUELEKEA DAR ES SALAAM/KARIAKOO DERBY NINI CHA KUJIULIZA?
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Andrea Ngobole Kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga sina mengi saana ya kuandika. ..lakini pia sio v...
Andrea Ngobole

Kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga sina mengi saana ya kuandika. ..lakini pia sio vema kuacha kuandika kidogo ili kuleta utofauti wa sahabiki na mfuatiliaji wa soccer..na Leo pengine kwanza niwape orodha ya Derby 16 bora barani Afrika..

MECHI ZA WATANI WA JADI AFRIKA
1. Algeria:
Hapa unawakuta JSM Bejaia na MO Bejaia . Mechi hii ni maarufu kwa jina la Algerian Clasico au Algiers Derby.

2. Angola:
Wababe Petro Atletico vs Primeiro de Agosto . Hii ni Derby maarufu na kongwe sana nchini Angolo wenyewe huiita Derbi de Povo.

3. Botswana:
Hapa kuna wakongwe Gaborone United na Township Rollers. Mechi hii hujulikana kama Gaborone derby.

4. Cameroon
Mechi hii ya watani wa jadi ni maarufu sana Afrika magharibi . Hapa unawakuta Canone Yaounde vs Tonnerre Yaounde.

5. Egypt:
Hii ndio derby namba moja Afrika ikiwakutanisha Al Ahly na Zamaleki . Inajulikana kama Cairo derby.

6. Ghana:
Asante Kotoko vs Hearts of Oak . Hii inajulikana kama Derby of Ghana.

7. Ivory Coast:
Hii ni derby ya pili kwa umaarufu Afrika magharibi inajulikana kama " Ivorian derby kati ya ASEC Mimosa na African Sports.

8. Kenya:
Hapa unawakuta Gor Mahia na AFC Leopards . Inajulikana kama Nairobi Derby inashika rekodi ya nne kwa umaarufu Afrika na namba mbili kwa Afrika mashariki .

9. Lesotho:
Great North Derby hapa unawakuta Linare FC vs Lioli FC . Ni mpambano wa jadi ambao huigawa nchi hiyo pande mbili kutokana na historia ya makabila ya nchi hiyo .

10. Mali:
Hii ni mechi ya saba kwa umaarufu Afrika katika orodha ya derby zenye msisimko kutokana na kuvuta hisia za wengi katika taifa hilo . Ni kati ya Djoliba AC vs AS Real Bamako . Wenyewe wameipa jina Grand Derby of Africa.

11. Morroco:
Hapa unawakuta vigogo FAR Rabat na watani wao Waydad Casablanca. Derby hii wameipa jina la Clasico Marocain .

12. Namibia:
Si maarufu sana hii derby kwa Afrika lakini ndani ya Namibia ina umaarufu mkubwa . Inajulikana kwa jina la Katutura Derby ni kati ya Black Afrika vs Orlando Pirates Windhoeik.

13. Nigeria:
Enyimba vs Kano Pillars . Hii inajulikana kama Kings Derby .

14. South Africa:
Hapa unawakuta Kaizer Chiefs vs Orlando Pirates. Hii ni derby namba mbili kwa ubora Afrika baada ya Cairo derby. Hii inaitwa Soweto Derby.

15. Tanzania:
Hapa unawakuta vigogo Yanga SC na Simba SC ikijulikana kama Dar es salaam Derby. Hii ndio Derby ya tatu kwa umaarufu Afrika na ya kwanza Afrika Mashariki.

16. Zambia:
Nchini Zambia kuna mechi mbili za watani wa jadi na zote zina umaarufu unaoshabihana . Ya kwanza ni Ndola Derby kati ya Zesco United na Forest Rangers. Ya pili ni Kitwe Derby kati ya Power Dynamos vs Nkana FC . Pia ndani ya jiji la Lusaka unawakuta Zanaco FC vs Lusaka Dynamo ikijulikana kama Lusaka Derby..


Sasa back to Kariakoo..hizi ni mechi ambazo hata kama ungekuja na hoja Kuntu kiasi gani, bado kuna watu wenye Team zao huwa wanaamini tu kuwa Zinapaswa zishinde by any means.
Simba wana kikosi kizuri, kikubwa na kipana. .hili ni kutokana na kusajili almost kikosi kizima katika dirisha la usajili. .hivyo ukichukua team nzima unapata vikosi viwili. .changamoto ninayoiona kwao japo mashabiki wake wasingependa kuisikia ni kuwa bado team haijawa organised. .
Wakati wa Maandalizi ya Msimu kabla ya jana jjmamosi Simba ilikuwa imecheza game 2 South Africa , game 2 Dar na Game 1 Zanzibar jumla ya game 5 ambazo safu yake ya ushambuliaji inayosifiwa na mashabiki wake imefunga jumla ya magoli manne kama sikosei. .ambayo sio idadi nzuri sana ikilinganishwa na kile tunachoambiwa.
Yanga imempoteza msuva Msimu huu pamoja na Haruna. .hawa ni wachezaji muhimu sana na katika mechi za Team hizi mbili ukiniuliza ningekuambia Msuva alikuwa anaperfome vzr kuliko Haruna. .
Hata hivyo kwenye safu ya ushambuliaji Yanga haijatetereka sana. .wana wachezaji ambao wamekaa kwa muda mrefu na wanajuana vema. ..hawahitaji kutengeneza combination maana wanayo tayari. .Tambwe, Ngoma, Emmanuel Martin wakisaidiana na Ajibu wanaweza kucheza vzr.
Upande wa kiungo Kamusoko na Mkongomani aliyekuja kuchukua nafasi ya Haruna watakuwa na kazi kubwa ya kupambana na viungo wa Simba waliomarika japo hawatacheza wote kama wanavyofanya kwenye friend matches.
Upande wa Beki sio mbaya sana japo kuna makosa niliyaona kwenye game ya Singida na Ruvu5shooting ambayo mwalimu atakuwa aliyaona na kuyafanyia kazi. .Yanga imecheza michezo mitatu ya kirafiki. .imeshinda miwili, imefunga mmoja imefunga magoli 5..so kama ni umahiri wa safu ya ushambuliaji tunaona kama bado wako vzr.
All in all utakuwa michezo mzuri ambao naamini matokeo yatapatikina ndani ya dakika 90. .lkn pia ni mchezo ambao huenda ukaondoka either na kocha mmojawapo au kufanya baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kwa mbwembwe kuanza kuandamwa na matusi kutoka kwa mashabiki wa kariakoo waliokosa uvumilivu.
Ni game ambayo chochote kinaweza kutokea, japo kwa jicho la kishabiki inaonekana kuwa Simba wana confidence zaidi ya ushindi kuliko Yanga. .na kwa amani ya kocha ,uongozi na wachezaji wapya waliosajiliwa wanapaswa kushinda kweli la sivyo yatawakuta makubwa...tusubiri dakika 90.
Nawatakia weekend njema.
B.Mshana

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top