PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WANAHABARI WAASWA KUTOANDIKA HABARI ZITAKAZOATHIRI UTALII NCHINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya vyombo vya habari katika sekta ya...



Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya vyombo vya habari katika sekta ya utalii kwa wahariri na wanahabari waandamizi katika mkutano wa sita ulioandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) mkoani Tanga.
VYOMBO vya habari nchini havipaswi kuandika mambo ambayo yanaweza kuathiri utalii wa Tanzania na badalayake vinapaswa kuwa chachu ya kukuza na kuutangaza utalii. 


Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas, amesema wanahabari wanapaswa kuhakikisha wanaandika mambo ambayo yataweza kuwavutia watalii kuja nchini na kutembelea vivutio mbalimbali hatua ambayo itasaidia kukuza pato la taifa.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari katika sekta ya utalii kwenye mkutano wa wahariri na wanahabari waandamizi wa kujadili sekta ya utalii nchini unaoendelea jijini Tanga.

"Tunaweza kutumia vyombo vyetu vya habari kuandika vizuri habari za utalii na sekta nzima ya utalii, kwa mfano Kenya huwezi ukakuta wanaandika jambo ambalo wanaona linaweza kuiathiri nchi yao," amesema Dk Abbas.

"Tuwafadhili Waandishi wa habari kufanya stadi muhimu kama habari za Takwimu (data Journalism) na za uchunguzi (investigative journalism) kwa habari zenye maslahi kwa Taifa kama vile kufichua mitandao ya Waharifu wa mazingira au Majangili",alisema Dkt Abbas.

Dkt.Abbas amewataka Wanahabari kuandika habari za Utalii kwa wingi katika suala zima la kuutangaza Utalii wa nchi yetu,ambao ukitangazwa vizuri itasaidia kukuza uchumi wetu na hatimae kuongeza pato la Taifa,akaongeza kuwa pia na jamii inayozunguka katika suala zima la utalii itanufaika kwa namna moja ama nyingine


Waandishi mbalimbali wa habari nchini wakisikilza mada wakati wa mkutano wa Hifadhi za Taifa, Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi nchini unaofanyika jijini Tanga.

 

Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. .

Pichani kati ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Dkt Ayub Rioba akiwa sambamba na Meneja Mahusiano wa TANAPA,Pascal Shelutete na wadau wengine wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas alipokuwa akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil  Makunga  akiwa na Wajumbe wengine katika Mkutano wa Wahariri na Waandishi waandamizi  ulioandaliwa na Tanapa
Wahariri na Waandishi waandamizi wa Habari walioshiriki katika Mkutano Maalum wa Mwaka ulioandaliwa TANAPA juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda 
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mkoa wa Morogoro Lilian Lucas  akipitia jarida la Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro wakati wakati somo la umuhimu wa kuhifadhi na kutangaza utalii wa eneo hilo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda  akichangia jambo kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini, wakati wa mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil  Makunga  akiuliza moja ya swali kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini,katika mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top