PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TANZIA... BILIONEA MAARUFU JIJINI ARUSHA NA MILIKI WA IMPALA, NAURA NA NGURDOTO HOTEL AFARIKI DUNIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini. Akizungumza na Mwana...

Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwananchi ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha.

Akihojiwa na gazeti hili Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo.

Laswai, amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo.

Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top