Dkt.
Jane Goodal ambaye ni raia wa Uingereza alianza utafiti katika Hifadhi
ya Gombe mnamo miaka ya 60 akiwa na umri wa miaka 26.
Katika
utafiti wake amegundua mambo mengi ikiwemo jinsi Sokwe wanavyojitambua,
kuwa na hisia na jinsi wanavyoishi kwa ushirikiano kama walivyo
binadamu.
Akizungumza
katika hafla hiyo Dkt Goodal anasema wakati anaanza kufanya utafiti
ilikuwa vigumu Sokwe hao kumkaribia kwani walikuwa wanamuogopa na
ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kumuona mtu mweupe, lakini alifanya
jitihada hadi wakamzoea na kuanza kumsogelea na kumuona mtu wao wa
karibu.
Anasema alitumia mbinu mbalimbali kama vile kuwapatia ndizi na vyakula vingine hadi wakamzoea.
Wakati
wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Utalii katikati ya jiji la
Dar es Salaam, viongozi na wageni waalikwa walipata wasaa wa kuangalia
picha mbalimbali za matukio ya sokwe wakiwa na Jane Goodall.
Katika
utafiti wake amefanikiwa kuanzisha chuo na kutunga vitabu pamoja na
video zinazoelezea maisha yake na Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani
Kigoma.
Katika
hafla hiyo walihudhuria Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali
George Waitara, Mwanasiasa Mkongwe Getrude Mongela, Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo cha Goodall, Mhe. Lembeli pamoja na mabalozi mbalimbali na
waalikwa wengine.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi
Dk. Jane Goodall tuzo maalumu kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa
miaka 60 wa maisha ya Sokwe pamoja na uhifadhi wa wanyama wengine
kwenye hifadhi ya Gombe, mkoani Kigoma katika hafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam leo. Tuzo hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
(Tanapa).
Dk. Jane akikabidhiwa cheti cha kutambua mchange wake kwa Tanzania kwa kuhifadhi Sokwe na wanayama wengine |
Jane akipatiwa pia zawadi ya kinyago cha Sokwe
Jane akikabidhiwa picha ya Sokwe
Mama Mongela akimvisha Jane zawadi ya vitenge
Dk Jane akitoa maelezo kuhusu maisha ya Sokwe
Waziri Maghembe akipata maelezo kuhusu maisha ya Sokwe yalivyo
Wasanii wa Tanapa wakitumbuiza kwa wimbo
Mwenyekiti
wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Mjeshi Mstaafu, Jenerali Waitara akitoa
shukrani nyingi kwa Dk Jane kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuiletea
Tanzania sifa lukuki duniani
Wageni
waalikwa wakisikiliza kwa makini wakati Waziri Maghembe akihutubia
katika hafla hiyo, ambapo alisema kuwa Dk. Jane ambaye wakati anaaza
utafiti yeye alikuwa darasa la pili, lakini utafiti wake umeiletea sifa
kubwa Tanzania na utakuwa ni urithi wa kipekee maishani
Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini
Profesa Magembe akihutubia katika hafla hiyo ya kumpatia tuzo Dk. Jane
Baadhi ya mabalozi waliohudhuria hafla hiyo
Dk Jane akielezea historia yake na jinsi alivyofanikiwa kufanya utafiti huo wa sokwe
Lembeli akitoa neno la shukrani
Jane akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi waliohudhuria hafla yake pamoaja na viongozi mbalimbali
Jane akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari baada hafla kumalizika
Post a Comment