Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipeana
mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB , Ineke Bussemaker (kulia)
baada ya kupokea mfano wa hundi wa gawiwo la shilingi bilioni 16.5
ambazo Serikali kama mwanahisa imepata katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya Benki hiyo ambayo kwa mwaka
ulioishia Disemba 31,2016 ilipata faida ya shilingi bilioni 153.8 licha
ya changamoto za kibenki, likiwa ni ongezeko la asilimia 2,
ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo ilipata faida ya shilingi bilioni
150.3.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Isdor Mpango (Mb) akiishukuru Benki ya
NMB kwa kutoa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali wakati wa
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Wanahisa
wa Benki ya NMB wakiwa katika Mkutano wao Mkuu wa Mwaka ambapo
uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imetangaza jumla ya
shilingi bilioni 52 kama gawiwo kwa wanahisa wote. (Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja-WFM
Benki
ya NMB imepata faida ya ya shilingi bilioni 153.8 kwa mwaka 2016 hivyo
kuiwezesha kutoa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali ambayo
inamiliki asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) alikabidhiwa hundi
kifani ya gawiwo hilo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa wa Benki
hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Mpango amezipongeza juhudi za watendaji wa Benki hiyo waliofanikisha
kupatikana kwa faida iliyowezesha Serikali kupata gawiwo. Aidha,
Serikali inajivunia mafanikio makubwa ya kiutendaji ya NMB na uwekezaji
wake ambao unatija na unaifanya serikali isijutie uamuzi wake wa
kuibinafsisha Benki hiyo.
Amesema
fedha hizo zilizopatikana kutokana na gawiwo zitaelekezwa kwenye
maendeleo ili kutatua baadhi ya kero zinazowakabili wananchi.
Ameahidi
kuwa, Serikali kama mwanahisa itaendelea kuitumia Benki hiyo kikamilifu
katika huduma za kibenki ili kuiwezesha kuongeza mapato.
“Shughuli
ambazo Serikali itazifanya kupitia NMB Bank Plc ni pamoja na malipo ya
mishahara ya wafanyakazi wa Umma na pia kukusanya mapato ya Serikali
yanayotokana na kodi na yasiyo ya kodi.
Waziri
Mpango ametumia nafasi hiyo kuagiza kampuni ambazo zenye ubia na
Serikali kuiga mfano wa NMB Benki Plc na kupeleka gawiwo katika faida
wanayopata.
“Katika
Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
haiingii akilini kusikia kila mwaka mnapata hasara lakini mpo hamtoki,
tumevumilia vya kutosha sasa imetosha, haiwezekani unawekeza miaka 10
lakini watanzania hawapati chochote” alionya Dkt. Mpango.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker amesema
jumla la gawiwo lote litakalolipwa kwa wanahisa ni shilingi Bilioni 52
kiwango ambacho kinaendana na sera ya Benki ya kutoa theluthi moja ya
asilimia 33.3 ya faida baada ya kodi kwa wanahisa wake.
Bussemaker
alisema kuwa mafanikio ya Benki hiyo katika mwaka ulioishia Disemba
31,2016 ilipata faida ya shilingi bilioni 153.8 licha ya changamoto za
kibenki, likiwa ni ongezeko la asilimia 2, ukilinganisha na mwaka 2015
ambapo ilipata faida ya shilingi bilioni 150.3
Wanahisa
wa Benki hiyo wamekubaliana kubadili jina la Benki hiyo kutoka National
Microfinance Bank na kuwa NMB Bank Plc. Waziri mpango amesema
mapendekezo ya kubadili jina yalifika Serikalini na Serikali imeridhia.
Hii
itakuwa mara ya pili kwa Serikali kupata gawiwo kutoka Benki ya NMB
ambapo mwaka uliopita, Benki hiyo ilitoa gawiwo la kiasi kama hicho cha
shilingi bilioni 16.5 baada ya kutengeneza faida.
Post a Comment