Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa kwa mara ya
kwanza amezungumzia utawala wa Rais Dkt John Pombe Magufuli huku
akimpongeza utendaji kazi wake unavyokwenda.
Rais Mkapa alimpongeza kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa
na wenye vyeti vya kughushi vya taaluma na kazi, na akasema anasikitika
tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.
Mzee Mkapa aliyesema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo yake na Shirika
la Habari la Ujerumani (DW) ambapo miongoni mwa mambo mengi
aliyozungumzia ni utawala wa Rais Magufuli, uhuru wa vyombo vya habari,
masuala ya uchumi.
Alisema Mkapa kuwa, wenye vyeti feki au watumishi hewa walikuwa
wakiingizia serikali hasara wengine wakiendelea kukaa madarakani bila ya
kustaafu, hivyo lilikuwa ni jambo la lazima kufanyika ni kwa manufaa ya
taifa.
“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati
nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi
niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga
mkono kabisa,” alisema Mkapa.
Kauli hii ya Rais Mkapa imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt
Magufuli kuwaamuru watumishi wa umma 9,932 waondoke kwenye utumishi wao
baada ya kubainika kughushi vyati vyao.
Post a Comment