Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia)
akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kilimo ili kukuza uchumi wa
viwanda alipofanya Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha
la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa tatu kushoto), katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akielezea
kuhusu ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) ambapo
alisema itasaidia kuchochea maendeleo si tu kwa Tanzania bali na nchi
jirani, wakati wa Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha
la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu
ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.
Naibu
Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto)
akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), (hayupo pichani) kuhusu nia ya Shirika hilo kufungua fursa zaidi
za mikopo kwa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa nne kushoto) na
Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa
nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa
Mkutano kati yao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar
es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang
(kushoto) wakiagana baada ya kumaliza mkutano kati yao, katika Mkutano
huo Zhang aliipongeza Serikali kwa hatua nzuri za ukuaji wa Uchumi.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
Prof. Benno Ndulu (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika,
Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) baada ya kumalizika kwa Mkutano kati
ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang
katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja, WFM
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang ameahidi kufungua madirisha ya
mikopo kwa nchi ya Tanzania kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na
Serikali za kukuza uchumi.
Bw. Zhang aliyasema hayo
alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika ofisi za Wizara hiyo Jijini Dar es
Salaam.
“Shirika la Fedha la Kimataifa
limeziona jitihada za kukuza uchumi wa nchi ambapo mpaka sasa Tanzania
inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki na ipo juu ya wastani wa
ukuaji wa uchumi Barani Afrika” Alisema Bw. Zhang.
Ameishauri Serikali kuendelea
kushirikiana na Sekta binafsi katika ukuaji wa Uchumi ili uchumi huo
uwe endelevu. Aidha ameitaka Serikali kuwa na mfumo shirikishi wa
kifedha utakao wanufaisha wananchi wengi.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amesema kuwa juhudi za Tanzania kwa
sasa ni kuchochea ukuaji wa Kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija.
“Umasikini haujatatuliwa kwa
kiwango ambacho Serikali ingependa kukiona, kwa kuwa mpaka sasa watu
walio katika umasikini na ukosefu wa huduma za lazima ni takribani
asilimia 34.4 “, aliongeza Dkt. Mpango
Kama nchi imeamua kwenda kwenye
uchumi wa kati na jambo ambalo linatiliwa mkazo ni upatikanaji wa umeme
wa kutosha na wenye bei nafuu .
Amesema kuwa Serikali imefanya
juhudi za kupeleka umeme mpaka vijijini lakini bado kazi hiyo
haijakamilika. Pia suala la miundombinu ya ya usafirishaji ni
changamoto, ukiwemo usafiri wa reli kutoka Mashariki hadi Magharibi mwa
nchi ambao ni wazamani na umeharibika.
“Serikali imeamua kujenga Reli
yenye kiwango cha Kimataifa (Standard gauge) ambayo ni ya gharama, na
kwa makadirio ya awali zinahitajika Dola Bilioni 7.6, lakini
umechukuliwa uamuzi huo ili kuharakisha Maendeleo”aliongeza Dkt. Mpango.
“Tayari tumeanza ujenzi wa reli
hiyo kwa fedha za ndani kwa takribani Kilometa 200 kutoka Dar es salaam
mpaka Morogoro na tutaendelea na ujenzi kadri fedha zinavyo patikana”
alifafanua Waziri Mpango .
Amesema kuwa, kumekuwa na tatizo
la ahadi za Wahisani kutotekelezwa kwa wakati jambo linalofanya baadhi
ya shughuli za maendeleo kutotekelezwa kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23
za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba, alisema ni vema Serikali ikaendelea
kuangalia vipaumbele katika ujenzi wa miundombinu ili iweze kuchochea
uchumi.
“Suala la ajira hasa kwa vijana
linatakiwa kufanyiwa kazi na pia kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na
ufanyaji biashara kwa Sekta Binafsi kwa kuwa Sekta Binafsi imekuwa na
mchango mkubwa katika Maendeleo kwa nchi nyingi Duniani” Alishauri Bw.
Mkwezalamba.
Ameishauri Tanzania kuendelea
kuwekeza kikamilifu katika Sekta ya Elimu kwa kuwa ni moja ya eneo
ambalo kama likifanyiwa kazi kikamilifu litaleta Matokeo chanya na ya
haraka katika ukuaji wa Uchumi.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hizo,
Waziri Mpango, amesema Serikali imeendelea kuhakikisha kunakuwa na
viwanda vingi ili vijana wengi waweze kupata ajira. Aidha tayari
Tanzania imeanza kutekeleza Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi
kidato cha nne ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kupata elimu.
Post a Comment